Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, April 11, 2014

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AKUTANA NA WADAU WA MICHEZO KILIMANJARO

 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw. Leonidas Gama akizungumza na wadau wa michezo mkoani Kilimanjaro.

Mwenyekiti wa chama cha soka manispaa ya Moshi Japhet Mpande akichangia hoja katika kikao cha wadau wa michezo Kilimanjaro.

Kocha wa timu ya Kitayoso FC, Hamad Haule akiongea kwa msisitizo.

Mjumbe wa kamati ya mashindano ya ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa Kilimanjaro akichangia hoja katika kikao.
 
Mdau wa zamani katika soka ambaye pia ni Kamishna wa michezo ya ligi kuu Kikwamba akichangia hoja.
 
Katibu wa Chama Cha Soka mkoa wa Kilimanjaro bwana Mohamed Musa akitoa ufafanuzi juu ya mchezo wa soka mkoani Kilimanjaro.

Makamu mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa bwana Darabu almaarufu kama born leader akitoa neno la shukrani kwa mkuu wa mkoa na wadau waliohudhuria katika kikako.

 Wadau waliokuwa katika meza kuu katika kikao cha wadau wa michezo mkoa wa Kilimanjaro.

 Baadhi ya wajumbe walioshiriki kikao cha wadau wa michezo mkoa wa Kilimanjaro.

Baadhi ya wadau mchezo wa soka kutoka kushoto ni Abdalah, akifuatiwa na Ismail, pamoja na wadau wengine waliohudhuria katika kikao.

 Baada ya kikao wadau wa michezo walipata kikombe cha chai na viafunwa.

Baada ya kikao na kupata kipooza njaa, wadau waliweza kujadiliana mawili matatu pamoja na kupeana pongezi.

MOSHI mkuu wa mkoa wa Kilimanajaro Mh. Leonidas Gama alikutana na viongzi pamoja na wadau wa michezo mbalimbali katika mkoa wa Kilimanjaro. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu mkoa wa Kilimanjaro. Kikao hicho kilifanyika tarehe 10 April 2014 na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka maeneo mbalimbali ya mkoani Kilimanjaro.

Dhumuni la kikao hicho lilikuwa ni kuzungumzia maendelo ya michezo katika mkoa wa Kilimanjaro ikiwepo viwanja vya mpira, club mbalimbali za michezo, mtandao ya michezo katika ngazi za wilaya na jinsi ya kuweza kuimarisha michezo na kuhakikisha michezo inapewa kipao mbele na pia kuweza kuandaa wanamichezo kuanzi wakiwa na umri mdogo ili kuweza kuwa na wanamichezo bora katika mkoa wa Kilimanjaro.

Baada ya wadau mbalimbali kuchangia hoja, likaibuka swala la viongozi wa michezo kuhujumu baadhi ya timu ili kuweza kuipa timu flani ushindi. Jambo hili lilikemewa vikali sana na mkuu wa mkoa Bw. Leonidas Gama kwa kusema “Kama mnataka mkoa ufike mbali kimichezo ni vyema mkahakikisha kuwa timu inayoshinda kwenye mashindano ni timu yenye uwezo na hata ikienda kwenye ngazi za juu itaweza kuendelea kufanya vizuri zaidi, lakini kama viongozi na waamuzi mkiipendelea timu fulani haitaweza kufika mbali” 

Mbali na hayo aliongeza kwa kusema "Nipo kwenye mazungumzo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusu kujenga uwanja wa michezo wa kimataifa katika eneo la wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro na eneo hilo limeshapatikana na lina ukubwa wa hekari 20, aliongeza kwa kusema TFF pia wanataka kuweka nyasi za bandia katika uwanja wa Kumbukumbu ya Mfalme George (Memorial)"

 Na kama inavyofahamika palipo na wazee hakuwezi kuharibika jambo kwa maana hiyo wakawekana sawa na kuahidiana kujenga umoja katika michezo ili kuweza kufikia malengo.

No comments:

Post a Comment