Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, April 16, 2014

PANONE FC YAVUNJA REKODI YA MIAKA 23 KWA KUWALETA YANGA MKOANI KILIMANJARO

Kutoka kushoto ni Katibu wa Chama Cha Soka mkoa wa Kilimanjaro Bw. Mohamed Musa akifuatiwa na Muwakilishi wa Panone Gido Marandu...

 Mgeni rasmi alikuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
Bw. Leonidas Gama akiwa katikati ya waliokuwa wamekaa jukwaa kuu wakifuatilia mpambano kwa makini sana.

Wachezaji wa Panone FC na YANGA wakisalimiana muda mfupi kabla ya mechi kuanza. 


Mgeni rasmi akisalimiana na wachezaji wa Panone FC.

Mgeni rasmi akisalimiana na wachezaji wa YANGA.


Mechi ikaanza na zifuatazo ni picha za mechi ilivyokua.



Gooo.! Mchezaji wa Kimataifa Didie Kavumbagu anaipatia YANGA bao la kwanza kipindi cha kwanza dakika ya 9






Gooo.! Mrisho Ngassa anaipatia YANGA goli la pili katika kipindi cha kwanza dakika ya 25.






Benchi la ufundi la Panone FC.

 Benchi la ufundi la YANGA.



Msemaji wa timu ya Panone FC, Cassim Mwinyi akiongea na waandishi wa Habari muda mfupi baada ya mechi kuisha.


Mabingwa wa mkoa wa Kilimanjaro ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa Panone FC maarufu kama matajiri wakutupwa walifanikiwa kuileta timu ya YANGA mkoani Kilimanjaro na kucheza nayo mechi ya kirafiki katika uwanja wa Ushirika jana tarehe 15 April 2014, mechi hiyo iliyohudhuriwa na maelfu ya mashabiki wa soka mkoani Kilimanjaro akiwemo mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw. Leonidas Gama.

Mechi hiyo ilikuwa na shamra shamra nyingi kutoka kwa wapenzi wa soka mkoani Kilimanjaro kwa kuwa ni muda miaka zaidi 23 imepita bila timu ya YANGA kucheza mkoani Kilimanjaro. Hii ilipelekea watu wengi sana kufurika uwanjani kwenda kushuhudia mtanange huo ambao ulikuwa wa kukata na shoka. Mpira ulianza kwa kasi sana na timu ya Panone FC ilionesha kuusoma mchezo wa YANGA.
 
Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika matokea yalikuwa YANGA-2, Panone FC-0, ambapo bao la kwanza lilifungwa na Didie Kavumbagu katika dakika ya 9 na bao la pili lilifungwa na Mrisho Ngasa katika dakika ya 25. Lakini waliporudi katika kipindi cha pili katika dakika ya 47 Hussein Jabu alifanikiwa kuongeza bao la tatu kwa upande wa YANGA,  na hadi mwisho wa mchezo ubao wa matokeo ulionesha YANGA-3, PANONE FC-0. 

Lakini ikumbukwe kuwa YANGA ni timu inayocheza ligi daraja la kwanza na Panone FC ni timu inayocheza ligi daraja la tatu na kwa walioshuhudia mchezo ule watakuwa mashahidi kuwa timu ya Panone FC ilijitahidi sana na ilionesha uwezo mkubwa sana kwanza kudhubutu kucheza na timu kubwa kama YANGA na pia uwezo wa wachezaji wa Panone FC walipokuwa uwanjani.  

Kwa upande wa msemaji wa Panone FC, Bwana Cassim Mwinyi alisema >> "Wachezaji wa Panone FC wameonesha uwezo mkubwa sana maana YANGA walitegemea wanakuja kukutana na timu ya kawaida sana na kama ulitazama katika kipindi cha pili timu ya Panone iliweza kuleta upinzani mkali sana kwa kikosi cha YANGA mpaka kupelekea kocha wa YANGA kusimama na kuanza kufokea wachezaji wake. Na huu ni mwanzo tu kwa timu ya Panone kuhakikisha tunafanya vizuri na kuleta upinzani mkubwa katika soka ndani ya Tanzania"  

Hata hivyo Shukrani za Dhati ziende kwa Kampuni ya Panone and Co. Ltd kwa kuwezesha kuivunja Historia hii. Ni takribani miaka 23 sasa toka Timu ya Ushirika moshi kuweza kucheza na Timu kubwa ya Yanga tokea kipindi hicho wakazi wa Mkoa wa kilimanjaro hawakuwahi kupata fursa ya kushuhudia mechi kubwa ndani ya mkoa huu. Kampuni ya Panone and Co. Ltd inayojishughulisha na Uuzaji Usambazaji wa Mafuta ya Magari Jumla na Rejareja Afrika Mashariki na kati  ikiwa kwa sasa imejikita katika biashara mbalimbali kama za uzalishaji wa mikate ya Panone Bread, ufungaji wa Korosho bora zenye nembo ya Panone, Cake na Maandazi ambavyo kwa Sasa bidhaa hizo zimejizolea Umaarufu mkubwa ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro kutokana na Ubora. Pamoja na Hayo Panone and Co. Ltd wana Hotel ya Kisasa iliyopo sakina kwa Iddi Jijini Arusha iliyokua ikiitwa 4js Hotel ambayo kwa sasa inaitwa Panone Garden Hotel na huku wakimalizia Ujenzi wa Hotel ya Kisasa iliyopo King'ori kilometa Chache kutoka uwanja wa ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA). na Ndio Wamiliki wa Timu hii ya Panone Football Club ambayo ni mabingwa wa Mkoa wa kilimanjaro na inatarajia Kuuwakilisha mkoa wa Kilimanjaro katika Ligi Daraja la Pili inayotarajia kuanza mapema Mwezi huu.

No comments:

Post a Comment