Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, April 23, 2014

FAHAMU AINA MPYA YA UTAPELI INAYOITWA "UKAGUZI WA FEDHA"

Stand kuu ya Moshi ya mabasi yaendayo mikoani.

MOSHI katika hali ya kustaajabisha katika siku za hivi karibuni kumeibuka utapeli wa fedha wa aina yake na kama mtu hufahamu ni rahisi sana kutapeliwa na watu hawa ambao wanaonekana kuwa na ujanja mkubwa sana. Na hata jana tarehe 22 april 2014 majira ya mchana maeneo ya stand kuu ya mjini Moshi ya mabasi yaendayo mikoani walitokea vijana wawili waliomfuata mtu aliyekuwa amesimama eneo hilo la stand na alidaiwa kuwa ni abiria. 

Matapeli hao wawili walimfuata na kujitambulisha kwa abiria huyo kuwa wao ni wakaguzi wa fedha na kuna fedha zimeibiwa mahali na ndio wanapita kukagua fedha hizo. Abiria yule kwa woga na bila kufahamu kuwa wale ni matapeli aliingiza mkono mfukoni na kutoa kiasi cha shilingi elfu sabini (70,000) na kuwakabidhi wale matapeli. 

Baada ya kuwakabidhi fedha zile malimuamuru abiria yule waende nae katika kituo cha polisi kilichopo karibu na stand kwa ajili ya ukaguzi wa fedha zile, lakini yule abiria alionesha kuogopa ndipo matapeli wale wakamwambia asimame pale pale ili wao waende polisi na watarudi muda si mrefu baada ya kupata uhakika kama fedha zile ndio zilizoibiwa ama laa?

Lakini baada ya wale matapeli kutokomea pasipojulikana ndipo abiria yule aligundua kuwa tayari ameshatapeliwa na kuanza kuomba msaada kwa wasamaria wema walikuwa maeneo ya pale stand. Lakini hakukuwa na namna ya kumsaidia zaidi ya kumwambia kuwa wale walikuwa matapeli na kwa sasa hawezi tena kuwapata.

Na kwa watu ambao ni wazoefu wa stand kuu ya mabasi ya Moshi walisema sasaivi aina hiyo ya utapeli ndio imekua ikitumika sana na matapeli katika eneo ya stand kuu na mabasi Moshi. 

Tahadhari kwa yeyote yule popote ulipo epukana na matapeli wanaofanya ukaguzi wa fedha zilizoibiwa, maana hakuna ukaguzi wowote unaofanyika kwa njia hiyo. Huo ni utapeli na ni vyema kuwafahamisha ndugu, jamaa na marafiki ili wasitapeliwe kwa njia hiyo ya ukaguzi wa fedha.

Unaruhusiwa ku'share habari hii na watu wengine wafahamu.


No comments:

Post a Comment