Samwel Sitta
Leo
kikao cha bunge maalum la katiba kimeshindwa kuendelea baada ya
kukatika kwa matangazo ya moja kwa moja kupitia televisheni ya Taifa na
kulalamikiwa na wajumbe kundi la wachache wanaotaka serikali tatu ambapo
taarifa yao ya kamati namba nne ndio ilikuwa ikiwasilishwa.
Mwenyekiti
Samwel Sitta alisema lengo la bunge kuingia mkataba na TBC ni kutaka
Wananchi waone kila kinachotokea ndani ya bunge ili kuwezesha kupatikana
kwa katiba bora ambayo mwisho wa siku Wananchi wataipigia kura ili
kutoa maamuzi ndio maana akatoa tangazo la kusitisha kikao.
Alisema
‘kwa sababu yoyote ile hatuwezi kuendelea, natoa maelezo tusikilizane…
natoa maelekezo kwa katibu kuangalia muda ilipozimika na Mh. Tundu Lissu
alikua anaongea ili Jumatatu tutakapo rejea nimpe Lissu nafasi ya
kwanza kuweza kumalizia’
Baada
ya Tundu Lissu kuanza kuongea na matangazo ya live kwenye TV (TBC)
kukatika, yalianza kutoka malalamiko kwamba yamekatwa makusudi ili
kuvunja nguvu ya maoni ya wachache wanaozitaka serikali tatu.
Nje
ya ukumbi wa bunge katibu wa baraza la habari Tanzania (MCT) ambaye pia
ni mjumbe wa bunge hilo Kajubi Mukajanga akatoa tamko kwa kusema "ni jambo la kusikitisha na la aibu, naongea kama Mjumbe na pia Katibu
wa baraza la habari… kitendo kilichofanyika leo mpaka hapo tutakapo
pata ushahidi kwamba kweli kulikua na tatizo la kimitambo"
"Ni
kitendo cha aibu na kuhujumu tasnia ya habari, haiwezekani mawazo haya
yakarushwa…… mawazo haya yasirushwe kwa sababu watu waliopewa majukumu
ya kusimamia kituo cha taifa (TBC) wanadhani kwamba hawayapendi mawazo
hayo" – Mukajanga.
Mwenyekiti
wa bunge maalum la katiba Samwel Sitta leo alikua katika wakati
mwingine mgumu hapa bungeni Dodoma baada ya kulazimika kutuliza wajumbe
wa bunge hili mara kwa mara wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya kamati
namba nne kuhusiana na sura ya kwanza na sura ya sita za rasimu ya
katiba mpya.
Hisia
hizo mara kadhaa zimekuwa zikiibuka miongoni mwa wajumbe pale
unapozungumziwa muundo wa muungano huku taarifa ya wajumbe wengi ikiunga
mkono muungano wa serikali mbili na wajumbe wachache wakiunga mkono
muundo wa shirikisho uliopendekezwa na tume ya mabadiliko ya katiba ya
kuwa na serikali tatu.
Licha
ya kutuliza hisia hizo pia mwenyekiti wa bunge alilazimika kumtaka
mmoja wa wajumbe wachache wa kamati namba nne kusoma maoni ya wachache
baada ya msomaji wa maoni ya wengi kukataliwa kusoma maoni hayo.
Namkariri Mh. Sitta akisema "kama unavyoona mwenyekiti wa kamati namba tatu unachokoza vurugu ndani
ya bunge na muda umefikia mwisho kwa hiyo malizia sasa, kwa kuwa
wachache mmemkataa mwenyekiti wa kamati namba tatu kusoma nawapeni
dakika 15 nyinyi wenyewe msome hayo mambo yenu"
Baada
ya ruhusa hiyo ya mwenyekiti, mjumbe Mchungaji PETER MSIGWA akapata
nafasi ya kuwasilisha maoni ya wachache na kutoa ufafanuzi kwa dadika 45
badala ya 30 zinazopendekezwa na kanuni za Bunge Maalum la Katiba.
Akiwasilisha
maoni ya wajumbe waliowengi wa kamati namba nne licha ya kukatizwa na
kelele za baadhi ya wajumbe mwenyekiti wa Kamati hiyo ameeleza kuwa ni
vigumu kuwa na shirikisho la serikali tatu kwani litadhoofisha au kuua
kabisa muungano.
Sehemu ya alichoongea akiwasilisha ni "hawa watu wanaosema hati ya muungano ni batili, kwanza ukishasema hati
ni batili manake muungano ni batili, manake bunge hili na jamuhuri ya
muungano ni batili, wanafanya nini humu? waondoke…!"
Source: Millardayo
No comments:
Post a Comment