Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, September 15, 2014

WAZIRI WA MAJI AANZISHA MFUKO KWAAJILI YA KUSAIDIA MAENDELEO YA VIJANA WA JIMBONI KWAKE

KILIMANJARO waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, amesema kuwa njia moja wapo na muhimu katika kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana ni kuwawezesha vijana kujiajiri wenyewe pamoja na  kupata miradi mbalimbali ya maendeleo.

Prof. Maghembe alisema hayo, wakati akizindua mfuko wa uwekezaji kwa vijana wilaya ya Mwanga, utakaojulikana kama Maghembe Youth Investment Fund utakaokuwa na makao yake makuu wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro.


Prof. Maghembe ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwanga, mkoani kilimanjaro, amesema kuwa  mfuko huo utakuwa chanzo cha vijana mbalimbali wilayani humo kufikia malengo hayo na kwamba kwa kuanzia mfuko huo utakuwa na shilingi milioni 100, ambapo Prof. Maghembe mwenyewe amechangia shilingi milioni 20 katika mfuko huo huku benki ya wananchi ya Mwanga ikiwekeza shilingi milioni 80 kwa ajili ya mfuko huo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa benki ya Mwanga,  Abby Ghuhia, Ofisa wa benki hiyo,  Abdhalla Msuya, alisema kuwa benki hiyo imelenga kuwafikia vijana zaidi ya 3,000 ili kuwapa elimu ya ujasiriamali.

No comments:

Post a Comment