Halmashauri ya manispaa ya Moshi, jiji la Arusha na jiji la Dar es salaam zimechaguliwa
kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya uhifadhi wa mazingira kwa mwaka 2015-2016.
Hayo yamebainishwa na mratibu wa shirika la kimataifa la uhifadhi
wa mazingira (WWF) Dr Teresia Olemako, wakati wa semina maalumu kwa wakuu wa
idara wa halmashauri ya manispaa ya Moshi iliyofanyika mjini Moshi ambapo
alisema kwa mwaka huu Tanzania itashiriki kwenye majaribio.
Alisema pamoja na kwamba mashindano hayo yana husu majiji, manispaa
ya Moshi imetajwa kuwa ni mdau mkubwa katika kushiriki kutokana na juudi zake
za muda mrefu za kutunza mazingira na kuweza kukabiliana, hivyo semina hiyo ni
kwajili ya kuwaanda wananchi wa halmashauri hiyo jinsi ya kushiriki .
Akifungua mafunzo hayo mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Shabani
Ntarambe alisema manispaa hiyo tayari ipo kwenye rekodi ya dunia kutokana na kufanya
vizuri katika swala la uhifadhi wa mazingira ukiwemo mlima Kilimanjaro.
Nae mbunge wa manispaa ya moshi Philemon Ndesamburo, amewataka
wananchi wa manispaa hiyo kutumia nafasi hiyo katika kuongeza kasi ya utunzaji wa
mazingir ili Tanzania iendelee kupeperusha bendera kimataifa katika swala
la utunzaji wa mazingira.
No comments:
Post a Comment