Mjumbe
wa Halmashauri kuu ya Taifa CCM, Agrey Marealle, amewataka vijana kujitokeza kwa
wingi katika kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa
unaotarajia kufanyika hivi karibuni.
Akizungumza katika mkutano wa umoja wa vijana wa wilaya ya Moshi mjini, uliofanyika katika kata ya Pasua Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, Marealle amesema kuwa ni wakati wa vijana kutumia fursa zilizopo ikiwa ni pamoja na uchaguzi huo kwa kushiriki chaguzi mbali mbali na kugombea nafasi mbali mbali za uongozi.
Marealle amewataka watanzania kuendelea
kuidumisha tunu ya nchi ili kusiwepo na machafuko ya umwagaji damu kutokana na baadhi ya vijana
wamekuwa wakihamasihwa kujitokeza katika maandamano na kusababisha kuwepo kwa
uvunjifu wa amani.
Kwa upande wake katibu wa vijana CCM,
wilaya ya Moshi Mjini, Joel Makwaiya amesema kumekuwepo na viendo vya kufanyiwa
vurugu na baadhi ya wafuasi wa vyama pinzani pindi mikutano hiyo ya CCM
inapofanyika.
Nae Mwenyekiti wa vijana CCM, wilaya ya Moshi, Abdallah Thabiti amewataka
vijana na wananchi kutokubali kurubuniwa na wanasiasa kutoka nje ya CCM, jambo
ambalo linapelekea kuwepo kwa vitendo vya uvunjifu wa amani.
Hata hivyo Mmoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani hapa, Ngangange mtenga, amewataka vijana, hususan wajasiriamali, kuacha tabia ya ubinafsi, badala yake wajiunge na vikundi ili waweze kupata fursa za kimaendeleo na kupatiwa mikopo kwa urahisi.
Mtenga aliongeza kuwa sifa ya sirikali ni kupeleka maendeleo kwa
wananchi wake hivyo akatumia fursa hiyo kuwataka vijana hao kuondokana na dhana
ya kuwa vibaraka wa kutumiwa na vyama vya upinzania kuwa vitawaletea maendeleo.
Mkutano huo pia , mjumbe wa Nec, alimsimika Edmund Rutaraka kuwa Naibu
kamanda wa vijana wilaya ya moshi mjini, ambapo amewaomba vjana hao kumpa ushirikiano
katika kukiimarisha chama hicho.
Katika mkutano huo, wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema
walifika wakiwa na gari aina ya Noah kwa lengo la kuvuruga mkutano huo, hata hivyo walidhibitiwa
na askari waliokuwepo katika mkutano huo.
No comments:
Post a Comment