KILIMANJARO jumla ya watoto
laki tano, wenye umri wa miezi tisa hadi miaka 15, mkoani Kilimanjaro,
wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya Surua na Rubella, katika wiki ya chanjo hiyo
iliyoanza Oktoba 18 na inatarajiwa kumalizikia oktoba 24 mwaka huu.
Akizungumzsa
na waandishi wa habari mkoni Kilimanjaro, Meneja Mpango wa chanjo Taifa, Dkt Dafrossa
Lyimo, amewataka wazazi, walezi pamoja na wataalamu wa afya kuhakikisha malengo
ya serikali ya kuwapatia chanjo watoto hayo yanafanikiwa kwa kiwango kikubwa.
Dkt Lyimo amewataka
wazazi hao kuacha tabia ya kuwazuiwa watoto wao, wasipatiwe chanjo hiyo, kwa dhana ya kuwa watoto hao wataua kizazi
chao.
Alisema
kuwa ugonjwa Surua na Rubella ni ugonjwa hatari, kwani huambukizwa kwa njia ya hewa, na kwamba hauna tiba kamili hivyo tiba yake ni kuwahi kupatiwa chanjo hiyo mapema.
Kwa upande
wake Mratibu wa Chanjo mkoa wa Kilimanjaro, Dkt Peter Kihamia alisema takwimu
zinaonesha kuwa jumla ya watu watatu wamebainiki kuwa na ugonjwa wa Rubella
kwa mwaka huu, kati ya vipimo 48 vilivyofanyiwa uchunguzi mkoani Kilimanjaro.
Alisema kwa
kipindi cha mwaka jana watu wapatao 28 wilayani Rombo waligundulika kuwa na
dalili za ugonjwa wa Rubella, na baada ya kugundua dalili hizo walizitibu.
No comments:
Post a Comment