Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, October 17, 2014

Kikundi cha VICOBA kinachoundwa na waandishi wa habari mkoani Kilimanjaro chakabidhiwa cheti cha usajili

KILIMANJARO wanachama wa benki za wananchi vijijini (Vicoba),  wametakiwa kuzitumia fursa zilizopo ili kujiletea maendeleo katika jamii ikiwa ni pamoja na uaminifu katika vikundi vyao na kuzingatia taratibu walizojiwekea.

Hayo yalisemwa na Meneja mahusiano wa benki ya CRDB, kanda ya kaskazini Godwin Maimu wakati alipokuwa akikabidhi cheti cha usajili kwa kikundi cha (Moshi Tanzanaite Vicoba Group),  kinachoundwa na baadhi ya waandishi wa habari  mkoani Kilimanajro.

Maimu aliwaasa wanachama wa vicoba kuwa waaminifu kwenye vikundi vyao kwa kurejesha mikopo kwa wakati ili kuwapatia fursa wengine kuweza kukopa.

Aliwataka kuzingatia taratibu na kanuni walizojiwekea ili vikundi vyao vizidi kuheshimika kwenye jamii na kuwapa nguvu kubwa kiuchumi.

Kwa upande wake kaimu Mwenyekiti wa Moshi Tanzanaite vicoba Group, Fadhili Athuman, alisema kuanzishwa kwa kikundi hicho kitasaidia kupunguza makali ya maisha kwa wanahabari hao.

No comments:

Post a Comment