NJOMBE serikali
imesema itaendelea kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya wazazi na
walezi ambao wanawaozesha watoto wa kike wanaohitimu elimu ya msingi na
sekondari badala yakuwaendeleza
kimasomo.
Kauli hiyo imetolewa
na mkuu wa wilaya ya njombe Bi. Sara Dumba
ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
mahafali ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya wasichana ya
Manyunyu iliyoko kata ya Matembwe wilayani humu Njombe Mashariki.
Aidha Bi. Dumba alisema bado wapo wazazi
ambao wanawaozesha watoto badala ya kuwapeleka shule hata kama wamechaguliwa
kuendelea na elimu ya sekondari ama elimu ya juu.
Awali akisoma taarifa
fupi ya shule hiyo mkuu wa shule Bi.
Neema Nzowa alisema wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo ya uchakavu wa mabweni na upungufu wa watumishi
.
Nao wanafunzi
waliohitimu kidato cha nne waliainisha changamoto zao mbele ya mgeni rasmi kuwa
baadi ya wazazi wanashindwa kuchangia chakula na michango mingine jambo ambalo
lina walazimu waalimu kuwarudisha wanafunzi majumbani kufwata michango hiyo.
No comments:
Post a Comment