Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, October 20, 2014

Mabadiliko ya mara kwa mara ya mitaala ya masomo ni changamoto kubwa katika elimu ya Tanzania

KILIMANJARO ukiukwaji wa maadili kwa vijana umetajwa kuwa changamoto kubwa inayoikabili shule ya sendari Shauritanga, iliyopo wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.

Uongozi wa shule hiyo umekiri wazi kwamba idadi kubwa ya vijana wanaosoma shuleni hapo, wameathiriwa na utandawazi unaowafanya kutaka kuingia na kuishi kwa tamaduni za kigeni.

Akizungumza katika mahafali ya 35 ya wahitimu wa kidato cha nne shuleni hapo, mkuu wa shule hiyo Kalist Shirima, alisema uongozi wa shule hivi sasa unakabiliwa na wakati mgumu kudhibiti ukiukwaji wa maadili kwa vijana wanaosoma shuleni hapo.

Shirima alisema kwamba uongozi wa shule umekuwa ukipokea malalamiko yanayotuhumu kuwanyima wanafunzi haki yao ya kidemokrasia pale wanapobanwa kufuata maadili, utamaduni wa kitanzania, kanuni na taratibu za shule hiyo.

Alisema suala hilo ni miongoni mwa changamoto kubwa zilizopo shuleni hapo, ingawa alikiri kuwa baadhi ya wanafunzi waliofanikiwa baada ya masomo wameweza kurejea shuleni hapo na kutoa ushuhuda wa mafanikio yao yaliyotokana na maadili waliyopokea shuleni hapo.

Aidha amezitaja changamoto nyingine kuwa ni mabadiliko ya mara kwa mara ya mitaala ya masomo, yanayochangia shule kufanya mabadiliko ya kila mara ya ununuzi wa vitabu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

Kwa upande wake mgeni rasmi wa mahafali hayo hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Rombo, Naomi Mwerinde, alizungumzia tatizo la ukiukwaji wa maadili kwa kutoa rai kwa vijana kujiepusha na makundi yanayochangia ukiukwaji wa maadili.

Alisema kitendo hicho kimekuwa kinagharimu maisha ya vijana wengi ambao wamekuwa wakipoteza maisha na wengine kutumikia vifungo gerezani.

Mahafali hayo yalihudhuriwa na viongozi wa kada mbalimbali, ambapo mgeni rasmi alikabidhi vyeti kwa wanafunzi 134 wanaohiti elimu ya kidato cha nne shuleni hapo mwaka huu 2014.

No comments:

Post a Comment