Naibu waziri wa ujenzi Mhandisi Gerison Lwenge, ambae pia ni
mbunge wa jimbo la Njombe Magharibi amekabidhi kiasi cha shilingi milioni
mbili kwa ajili ya kuendesha shule
pamoja na vitabu arobaini na tisa (49) vya
masomo mbalimbali vikiwemo vya
sayansi katika shule ya sekondari ya luduga iliyoko wilayani
wanging’ombe .
Akiwa katika ziara ya
siku kumi na nne wilayani wanging’ombe
mhandisi Lwenge alisema kwa
kutambua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu hapa nchini imemlazimu
kupeleka vitabu hivyo katika shule zote za
sekondari zilizopo katika jimbo lake ili wanafunzi waweze kujisomea na kuleta
ufaulu mkubwa katika masomo ya sayansi.
Aidha mhandisi Lwenge alisema katika mchakato wa rasimu ya katiba serikali
imepitisha kipengere cha elimu ya msingi kweda hadi kidato cha nne ambapo
itakuwa na mitaala ya masomo mbalimbali yakiwamo ya ufundi stadi na kilimo yanayowapa wanafunzi fursa ya kujitegemea
wanapohitimu elimu hiyo.
Katika hatua nyingine
mhandisi Lwenge aliwahakikishia wananchi wa vijiji vya kata ya Luduge na vijiji
vya Korinto, Kilonge na Mwambegu kupelekewa miundo mbinu ukiwemo umeme
mwaka huu ambapo vijiji vingine
vitapatiwa kwa awamu nyingine itakayofuata, nakuwataka wananchi watakao wekewa umeme kwa awamu hii kuweka maandalizi kwa ajili ya
umeme huo.
Akisoma taarifa fupi
ya shule hiyo mkuu wa shule ya Luduga alisema shule hiyo inakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa maji, upungufu wa nyumba za waalimu, mabweni, bwalo la chakula pamoja na maabara za kisasa.
No comments:
Post a Comment