Baadhi ya wazazi na
walezi mkoani Njombe ambao watoto wao
walikuwa wanasoma katika kituo cha chekechea na awali Ihungilo wamelalamikia kitendo cha mratibu
elimu kata ya Ihungilo, Bwana Lugumko Kienga kwa kuwahamisha watoto wao kutoka kituo hicho na kuwapeleka katika shule ya awali iliyopo katika shule ya
msingi Ihungilo.
Wakiongea kwenye mkutano wa wazazi na bodi ya kituo hicho
uliofanyika kituoni hapo walisema kuwa wameshangazwa na kitendo cha mratibu huyo cha kuwahamisha watoto wao bila ya ridhaa
yao.
Akizungumza na wazazi
na walezi wa watoto hao mwenyekiti wa
bodi wa kituo hicho Olasi Mkulo alisema idadi ya watoto waliohamishwa kutoka
kituo hicho ni watoto ishiri na tisa (29) ambapo amelaani kitendo hicho na kusema
kuwa kitendo alichofanya mratibu huyo hakikufwata utaratibu kwakuwa alitakiwa
kukutana na uongozi wa kituo hicho na
kukubaliana.
Kwa upande wa mratibu
elimu Bw. Kienga alisema kuwa imemlazimu kuchukua uamuzi huo kwani kituo hicho
hakijakidhi vigezo vya kituo cha awali na hakijakamilisha usajili wala hakina
vifaa vyakutosha kwa ajili ya
kufundishia.
Kituo cha chekechea na awali cha ihungilo kilichopo chini ya parokia ya uliwa kimeanzishwa mwaka 1998 ambapo hadi sasa
takribani watoto thelathini wanasoma katika kituo hicho.
No comments:
Post a Comment