KILIMANJARO jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mwalimu
mmoja wa shule ya sekondari Muungano baada ya kukutwa akifanya mapenzi na
mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule hiyo.
Akitoa taarifa hiyo jana kwa waandishi wa habari, kaimu
kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Koka Moita alisema tukio hilo lilitokea Oktoba
3 mwaka 2014, majira ya saa tano asubuhi katika mjini mdogo wa Himo wilayani
Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kamanda Moita alisema mwalimu huyo alifumaniwa na mwanafunzi
huyo akifanya mapenzi katika nyumba ya kulala wageni iliyojulikana kwa jina la
Kilimanjaro Gest House iliyopo katika eneo la Himo.
Akielezeea mazingira ya tukio hilo kamanda Moita alisema awali
mwalimu huyo alionekana akiwa amembeba
mwanafunzi huyo katika pikipiki ambapo
alikuwa akielekea katika nyumba hiyo ya kulala wageni.
Kamanda alisema baada ya wazazi wa binti huyo kugundua kuwa
mwalimu huyo alikuwa akimpeleka mwanafunzi huyo katika nyumba ya kulala wageni,
walimfuatili na kumkuta akiwa chumbani na mwanafunzi huyo wakifanya mapenzi.
Aidha alisema mwalimu huyo anashiliwa katika kituo cha polisi
Himo wilayani Moshi vijini, mkoani Kilimanjaro, na kwamba taratibu za
kisheri zitakapo kamilika atafikishwa mahakamani ili hatua zaidi za kisheria
ziweze kuchukuliwa dhidi yake.
No comments:
Post a Comment