KILIMANJARO wananchi wanaoishi mkoani Kilimanjaro wanalalamikia kukithiri kwa uchafu katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi husani katika maeneo ya masoko jambo ambalo limechangia kushusha hadhi na sifa ya mji wa Moshi.
Mji wa Moshi ambao unajulikana kwa kuongoza
kwa usafi nchini, mwaka huu ulishika nafasi ya pili hali ambayo wananchi hao
walisema imechangiwa na kukithiri kwa
uchafu katika kila kona ya Mji huo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwaandishi
wa matandao huu wa "Kilimanjaro Officia Blog" mjini Moshi baadhi ya wananchi hao walisema hali ya uchafu katika
maeneo mbalimbali ya mji Moshi inatisha ikilinganishwa na kipindi cha zaidi ya miaka
minne iliyopita.
Kwa mujibu wa wananchi hao walisema soko Kuu
la Mji wa Moshi lilifungwa na mamlaka ya chakula na dawa kutokana na uchafu uliokithiri
katika maeneo mbalimbali ya ukuuzia vyakula jambo ambalo limekuwa likihatarisha
afya za walaji.
Aidha walisema bado kumekuwa na mrundikano wa
uchafu na maji machafu kutiririka katika masoko mengi huku halmashauri ya
manispaa ya Moshi ikifumbia macho suala hilo na kuacha kuchukua taka hizo mara
kwa mara.
Akizungumzia suala hilo Kaimu Mkurugenzi katika Halmashauri ya
Manispaa ya Moshi Chirstoph Mtamakaya alikiri kuwepo kwa uchafu katika maeneo
mbalimbali ya manipsaa ya Moshi kutokana na kufutwa kwa sheria ndogo ya
mazingira.
Alisema kutokana hali ya uchafu kuendelea
kukithiri halmashauri hiyo imejipanga kuteresha sheria hizo za usafi ili
kuthibiti hali hiyo na hatima mji wa Moshi kuendelea kushika nafasi ya kwanza
kwa usafi nchini.
Alisema ujenzi wa soko kuu la Mjini Moshi
lililofungwa kutokana na uchafu na
mamlaka ya chakula na dawa nchi TFDA limeshindikana kujengwa kwa wakati
kutokana na ukosefu wa fedha .
Mtamakaya alisema manispaa hiyo imetenga
zaidi ya shilingi milioni 278 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2014/2015 kwaajili
ya ujenzi wa miundombinu na ukarabati wa
masoko ikiwa ni pamoja na ujenzi wa soko kuu la moshi.
No comments:
Post a Comment