Mgonjwa
huyo aliyefikishwa katika
Zahanati hiyo Juzi majira ya Jioni, ambapo hali hiyo ilisababisha huduma
za afya katika
zahanati hiyo kusitishwa kwa muda usiojulikana, ambapo wagonjwa
waliokuwa
wakipatiwa matibabu kutoka ndani na nje ya kata hiyo kuondolewa na
watoto waliokuwa wakipata chanzo katika zahanati hiyo walihamishiwa katika
ofisi
ya afisa mtendaji wa kata hiyo.
Taarifa za awali zinadai kuwa, mgonjwa ni Raia wa Tanzania mzaliwa wa Marangu wilayani Moshi, mwenye makazi yake jijini Dar es Salaam, alipokelewa katika uwanja wa ndege wa kimataifa Kilimanjaro (KIA), akitokea
nchini Senegal kikazi, ambapo alisafirishwa hadi kwenye zahanati hiyo baada ya
kudai kupatwa na maumivu makali ya kichwa.
Mgonjwa huyo (jina halijafahamika), ameendelea kutibiwa hospitalini hapo na wataalam wa afya waliopo
katika zahanati hiyo.
Aidha taarifa zaidi zinadai kuwa
wataalam wamechukua sampuli ya damu kutoka kwa mgonjwa huyo kwa ajili ya vipimo, ili
kujiridhisha, wakati huduma nyingine za matibabu zikiendelea kutolewa kwa
mgonjwa huyo anayedaiwa kusafiri kutoka nchini Senegal.
Aidha jopo la wataalam wa afya
likiongozwa na mganga mkuu wa mkoa Dk. Mtumwa Mwako, mganga wa manispaa ya Moshi
Dk. Christopher Mtamakaya pamoja na watendaji wakiongozwa na mkurugenzi wa
manispaa Shaban Mtarambe na viongozi wengine walionekana wakiendelea na kikao
katika eneo hilo la zahanati.
Alipohojiwa na waandishi wa habari
kuhusiana na tukio hilo, mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Shaban Mtarambe,
alisema hayuko tayari kuzungumza kwa maelezo kuwa suala hilo ni la kitaalam
zaidi linalohitaji waataalam wa kada ya afya kulizungumzia.
Jitihada za kina kumpata mganga mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro Dk. Mtumwa Mwako, kuweza kutolea ufafanuzi suala hilo
zilishindikana huku kukiwa na taarifa kwamba hakuwa tayari kulizungumzia mpaka
pale uchunguzi wa kina kuhusu mgonjwa huyo utakapokamilika.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa
Kigongoni kata ya Shirimatunda, Juma Sambeke, alithibitisha kuwepo kwa mgonjwa
huyo baada ya kupokea taarifa kutoka viongozi wa wenzake.
Mwenyekiti huyo alisema licha ya
mgonjwa kufikishwa katika zahanati hiyo, uongozi wa kijiji haukuwa na taarifa
huku akipokea majibu kutoka ngazi ya manispaa kuwa suala hilo linaratibiwa na
mkoa.
Naye diwani wa kata ya Shirimatunda
Felix Mushi, alilaumu uongozi wa manispaa ya Moshi, kwa uamuzi wake wa kutenga
eneo hilo kwa ajili ya wagonjwa wa ebola, jambo alilosema ni hatari kwa jamii
inayozunguka zahanati hiyo.
Diwani Mushi, alisema eneo hilo
limezungukwa na huduma zote za kijamii, ambapo baadhi ya wazazi wamekuwa na
mashaka hivyo kuzuia watoto wao kwenda shuleni.
Hata
hivyo waandishi wa habari waliofika eneo la tukio walishuhudia watoa
huduma za afya katika zahanati hiyo wakiingia na kutoka ndani ya jengo
alikolazwa mgonjwa huyo, ingawa baadhi yao hawakuwa na mavazi rasmi ya
kujikinga kama ilivyo kwa wataalam wanaotoa huduma katika nchi
zilizokumbwa na ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment