Wananchi wa kijiji cha
makachaula wilayani Njombe wamevamia
msitu wa asili nakuendesha shunguli za kiuchumi
kikiwemo kilimo hali ambayo inahatarisha vyanzo vya maji vinavyozunguka
msitu huo.
Akizungumza na kituo
hiki afisa mtendaji wa kata ya uwemba
chaazi kione katika mahojiano maalumu
amesema uharibifu mkubwa unatokana na shunguli za kilimo cha
umwagiliaji katika eneo la msitu huo na kusema kuwa watu ambao
wamebainika watachukuliwa hatua za
kisheria.
Aidha bw.kione
amewataka wananchi wanaoishi jirani na msitu
huo kuendelea kushirikiana na serikali za vijiji vyao katika kuwabaini
watu wanaokaidi agizo la serikali lakutokuendesha shunguli za kibinadamu kwenye
vyanzo vya maji pamoja na uharibifu wa mazingira.
Mkoa wa njombe ni
miongoni mwa mikoa iliyo na matukio mengi ya uharibifu wa mazingira kutokana na shunguli za kilimo
kwani baadhi ya wananchi huandaa mashamba kwa kuchoma moto.
Serikali kupitia
sheria ya utunzaji wa mazingira imepiga
marufuku uharibifu wa mazingira na kutokuendesha shughuli zozote za kiuchumi
kwenye vyanzo vya maji na kuwataka wananchi kuendesha shughuli hizo mita sitini
kutoka kwenye vyanzo hivyo.
No comments:
Post a Comment