Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, October 24, 2014

Wanachama 75 wa CHADEMA, wahamia CCM

       
KILIMANJARO wanachama  75 wa Chama cha Demokransia na Maendeleo (CHADEMA) akiwemo katibu kata wa kata ya Orkolili  Memei Laiza  wamkihama na kujiunga    Chama hicho na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya Siha mkoani Kilimanjaro.

Wakikabidhi kadi zao na kukabidhiwa kadi za CCM  katika hafla  ya uzinduzi wa kata Mpya tano za kichama ziliyofanyika mwishoni mwa wiki na kuongozwa na Mbunge wa Jimbo hilo Agrey Mwanri katika kijiji cha Donyomurwa
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Aliywekuwa mgombea udiwani wa kata ya Orkolili  kwa  tiketi ya CHADEMA  katika uchaguzi  mkuu  mwaka 2010, Jacksoni Saningo Laiza alisema kuwa  wamechoshwa na sera za Chama hicho zinazotawaliwa na wachache  na kukosekana na kwa dira ya maendeleo ya Chama hicho.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi kwenye mkutano huo,Laiza alisema awali alijiunga na chadema akitokea chama cha mapinduzi akidhani  chama hicho kina mashiko na wananchi badala yake mambo aliyoyakuta hayakuwa kama alivyotarajia.

Alisema hasa kikubwa kilichomfanya kukirudia chama hicho ni kutokana na utendaji makini unaofanywa na viongozi wa chama hicho ambao umepeleka kuweza kuzipatia ufumbuzi kero mbalimbali za wananchi.

Alisema, hamasa kubwa ya kukihama chama hicho na kuhamia CCM ni kutokana na  utekelezaji  wa vitendo wa shughuli za kimaendeleo katika kata  hiyo  ambayo kwa sasa imepata umeme ,maji ammbayo ilikuwa kilio kibwa kwa wananchi wa maeneo ya wakazi ya wafugaji.

Laiza alikabidhi vifaa mbalimbali, ikiwemo Katiba na miongozo mbalimbali  ya CHADEMA Bendera  tano ambazo zilikuwa zimetundikwa katika maeneo mbalimbali ya kata hiyo.

Awali akiwapokea wanachama hao, Mbunge wa jimbo hilo Mwanri aliwataka wanachama wanaohama chama chochote na kuhamia chama kingine kutokuchoma  au kuacha bendera ya chama kingine ili kuepuka migogoro kati ya chama na chama kingine.

Mwanri alisema kuwa idadi ya wanachama wakihama chama hicho ni ishara ya kusamabaratika kwa  CHADEMA kabla kufikia uchaguzi  ujao wa viongozi wa  serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais hapo mwakani.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Wilaya hapa Oscar Temi aliwataka vijana kubadilika na kuacha kukaa vijiweni badala yake waunde vikundi vya ujasiriamali vitakavyoweza kuwakwamua kimaisha.

No comments:

Post a Comment