KILIMANJARO mkaguzi wa shule za Sekondari Manispaa ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro, Mtenguzi Kidyamakuo, ametangaza nia yake ya kugombea Ubunge Jimbo la Handeni mkoani Tanga, katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani, ambapo Jimbo hilo kwa sasa linashikiliwa na waziri wa viwanda na biashara Dk. Abdhalla Kigoda.
Akitangaza nia yake hiyo ambayo amesema atagombea kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Mwalimu Kidyamakuo, amesema amefikia uamuzi kwa lengo la kuharakisha maswala ya kimaendeleo ambayo amedai kuwa yanasuasua.
Mwalimu Kidyamakuo amesema Jimbo hilo limekuwa na wabunge mbalimbali kwa zaidi ya miaka 20 sasa lakini hakuna maendeleo yeyote yaliyopelekwa katika jimbo hilo ambayo wananchi wake wanaweza kujivunia.
Amesema moja wapo ya changamoto ambazo atasishughulikia ni pamoja na Miundo mbinu ya Barabara na Maji ambapo amesema zimekuwa zimekuwa zikikwamisha wananchi katika juhudi zao za kujikwamua kiuchumi.
Amefafanua kuwa changamoto zingine ni ukosefu wa huduma za afya wananchi wa jimbo hilo wanalazimika kutembea kwa zaidi ya kilomita 30 kufuatilia huduma hizo huku waathirika wakubwa wakiwa ni watoto, wanawake na wazee.
Amevitajaja baadhi ya vijiji ambavyo vinakabiliwa na changamoto hizo kuwa ni pamoja na Kwa Magoma, Msente, Tilibe, Muumbiri, Mzindu, Kwa Mkono na Kwedikwazu.
No comments:
Post a Comment