KILIMANJARO halmashauri
ya wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro imepatiwa
msaada wa baiskeli 500 kutoka serikali ya Japani kwaajili ya kuwasaidia
watoto yatima, walemavu na wazee wasiojiweza ili waondokane na
changamoto mbalimbali za kimaisha
ikiwemo chakula, mavazi, matibabu .
Naibu waziri wa tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni mbunge wa
Siha Agrey Mwanri, aliyasema hayo wakati wa ghafla fupi ya makabidhiano ya
baiskeli hizo, yaliyofanywa na balozi mdogo katika ubalozi wa Japani, Bw. Kazuyoshi
Matsunaga .
Mwanri
alisema upatikanaji wa baiskeli hizo umetokana na
mausiano mazuri, ya halmashuri hiyo na jiji la Ibaraki la nchini Japani
na
kwamba zitauzwa na fedha zitakazo
patikana zitatumika katika kusaidia jamii wakiwemo yatima, walemavu na
wazee, badala ya kuitegemea serikali kufanya kila jambo.
Akikabidhi msaada huo balozi mdogo katika ubalozi wa Japani
Bw. Kazuyoshi Matsunaga alisema baiskeli hizo ni sehemu tu ya misaada
inayotarajiwa kuwasiliswa katika halmashauri hiyo na kwamba wanategemea
misaada hiyo italeta mabadiliko chanya
katika halmashuri hiyo.
Kwa mujibu wa bwana Mwanri alisema, miradi mingine
inayotarajiwa kutekelezwa kati ya jiji la Ibaraki na halmashauri ya Siha ni
upandaji miti kwa kasi ambapo mradi huo utapatiwa gari kwaajili ya kumwagilia maji kipindi cha kiangazi, pia gari la wagonjwa
kwaajili wa wananchi waishio pembezoni mwa wilaya hiyo, pamoja na gari la zimamoto.
No comments:
Post a Comment