Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu wadhifa wake kuanzia hii leo.
Taarifa ya Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais, Ikulu iliyotolewa jana na Mkurugenzi wake, Salva Rweyemamu
kwa vyombo vya habari imethibitisha kujiuzulu kwa Werema kuanzia jana. Alikuwa
kwenye wadhifa huo tangu mwaka 2009 alipochukua nafasi ya Johnson Mwanyika
aliyestaafu.
Taarifa hiyo imeongeza
kuwa, Rais Jakaya Kikwete amekubali ombi la kujiuzulu kwa mwanasheria huyo.
Rais
Jakaya Kikwete akimwapisha Jaji
Frederick Werema kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Sherehe ya
kumwapisha Jaji Werema ilifanyika Ikulu jijini Dar tarehe Novemba 6,
2010 ikiwa ni siku chache baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani kwa
awamu ya pili na kumteua tena kuendelea na wadhifa huo baada ya uteuzi
wa awali wa 2009. Wapili kushoto ni aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi,
Philemon Luhanjo na Katibu wa Baraza la Mawaziri.
Source: Mroki
Source: Mroki
No comments:
Post a Comment