KILIMANJARO jeshi polisi mkoani
Kilimanjaro linawasaka watu 10 wanaosadikiwa kuwa ni majambazi baada ya kuvamia
nyumbani kwa mtu mmoja na kupora mali mbalimbali ikiwemo bastola aina ya
Beretta yenye nambari E9B3K2Y.
Akizungumza na vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoani
Kilimanjaro Geofrey Kamwela alisema tukio hilo lilitokea Januari tano mwaka huu
majira ya 10:00 alfajiri katika kata ya Ngangamfumuni katika Manispaa ya Moshi
mkoani hapa.
Akielezea mazingira ya tukio hilo kamanda Kamwela alisema kundi
la majambazi hao walivamia nyumbani kwa Gervas Mulokozi (64) wakiwa na silaha
mbalimbali za jadi ikiwemo Mapanga, Marungu na fimbo na kisha kumshambulia na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili wake.
Alisema watu wengine walio jeruhiwa katika tukio hilo ni pamoja na mkewe Advenika Mulokozi (58) muuguzi katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro
Mawenzi na kujeruhiwa kwa kupiga marungu
kichwani na mkononi pamoja na mtoto wake Janath Mulokozi (25).
Alisema mara baada ya uwajeruhi kwa watu hao walifanikiwa
kupora bastola hiyo, Deki moja ya DVD, Simu sita za aina tofauti tofauti zenye
thamani ya zaidi ya shilingi laki nane, funguo za magari pamoja na vitu vingine
mbalimbali ambavyo thamani yake bado
haijajulikana.
Aidha alisema majeruhi wote wamelazwa katika hosptali ya
Mawenzi kwaajili ya kupatiwa matibabu zaidi na kwamba jeshi la polisi
linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wote waliohusika na tukio hilo ili
sheria iweze kuchukua mkondo wake.
No comments:
Post a Comment