Wanafunzi zaidi
100 wanaosoma katika chuo cha uuguzi cha
huruma"Huruma nursing college" wamelala katika stendi ya madasi ya rombo mkuu
baada ya kufukuzwa usiku na kuzuiliwa kuingia chuoni hapo na uongozi wa chuo
hicho kwa kushindwa kukamilisha ada.
Wanafunzi hao wamejikuta katika wakati mgumu usiku wa
januari 4 mwaka huu, baada ya kutimuliwa
na kuzuiwa kuingia katika eneo la chuo
kwa kile kinachoelezwa kuwa walishindwa kukamilisha ada zao na michango
mingine ya chuo.
Wanafunzi hao wanasema wamelazimika kulala katika stendi hiyo ya mabasi mkuu wakisubiri kutumiwa fedha na ndugu zao kwani wengi wao hawakua na fedha za kulipia sehemu ya kulala.
Mmoja wa wakazi wa rombo mkuu, Ester Tarimo, alisema "wanafunzi wa
chuo hicho walikuwa wakiranda randa ovyo usiku mitaani wakiwa na mabegi yao pamoja na vifaa vya shule kutokana na kufukuzwa usikuu huo na kukosa
sehemu ya kulala."
Tarimo alisema uongozi wa chuo hicho haukufanya vizuri
kuwafukuza wanafunzi hao usiku na kwamba
wangetumia busara wawarudishe asubuhi kwa kuwa kulikuwa hamna madhara yoyote ya
kuwaacha chuoni hapo.
Mmoja wa wanafunzi hao John Shija ambaye mzaliwa wa Mwanza,
alisema tarehe tatu ndipo aliporipoti
chuoni hapo akitokea nyumbani na kutimuliwa usiku huo kwa kuwa hakuwa amemaliza
kulipa ada.
Alisema aliwaomba uongozi huo kuwavumilia kwa kuwa wazazi wao
wangetuma fedha hizo lakini hawakuwasikiliza na kuwatoa nje na kuamuru mlinzi
kutoruhusu mwanafunzi kuingia chuoni hapo usiku huo.
“sisi tulifika hapa saa kumi na mbili jioni ya tarehe 3
tukaambiwa hakuna ruhusa ya kuingia chuoni tukaambiwa tusubiri ilipofika saa mbili usiku tukafukuzwa tukawaomba kwamba tumeshawapigia wazazi wetu simu wanatuma hela lakini hawakutaka kutusikiliza kabisa” alisema mmoja wa wanafunzi hao.
Aidha walisema kuwa kwa sasa wanaishi kwa shida kwani wengi wao hawana uwezo wa kulipia nyumba ya kulala na pia kurudi kwao ni mbali “mimi natokea mkoa wa mwanza tangu tarehe 3 nipo hapa siwezi kurudi kwetu ni mbali na hela ya kulipia nyumba ya wageni sina sijui nitafanyaje naomba tusaidiwe jamani”alisema Shija
Walisema utaratibu huo wa kulipa ada kwanza ni mpya na kwamba wazazi hawakushirikishwa kuhusu utaratibu wa ulipaji wa michango ya shule ili kuepusha usumbufu usio wa lazima kwani wazazi ndio wangetakiwa kulipa na sio kuadhibu wanafunzi.
Akizungumzia suala hilo Kwa niaba ya Mkuu wa Chuo Hicho sista Evarista Lasway ambaye imeelezwa kuwa ni Mgonjwa mwakilishi wa Mkuu huyo wa Chuo Sista Florence, amekiri kufukuzwa kwa wanafunzi hao ambapo alisema kuwa ni utaratibu ambao walijiwekea na wanafunzi hao kabla ya
kufunga chuo na hivyo sio suala la kushtukiza.
Sista Florence alisema
kuwa wazazi wa wanafunzi hao walipewa walishirikishwa kuhusiana na maamuzi mapya ya
bodi ya chuo hicho waliwapigia simu wazazi na kuwaeleza kuwa wawasilishe kwa wakati michango ya chuo na walioshindwa kufanya hivyo ndio
walioofukuzwa.
No comments:
Post a Comment