KILIMANJARO Mashindano
ya 13 kimataifa
ya riadha ya Kilimanjaro marathoni mwaka 2015
ya mezinduliwa rasmi mkoani Kilimanjaro ambapo Tanzania imetamba kuwa
itag’ara katika mashindano hayo yanayo tarajiwa kufanyika mwezi machi
mwaka huu mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza
kwa niaba ya raisi wa chama cha riadha nchini kwenye
uzinduzi wa mashindano hayo uliyofanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, mwenyekiti wa chama
cha riadha
mkoani Kilimanjaro Listone Metacha alisema Tanzania imewaanda vilivyo
wachezaji wake mapema badala ya kukurupuka katika dakika za
mwisho.
Akizindua mbio hizo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
leonidas Gama, katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro
Severin Kaitwa, amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika kushiriki mashindano
hayo, ambayo mbali na kuchangia uchumi wa nchi ya Tanzania, pia yanaipa sifa kubwa kimataifa.
Meneja wa bia ya Kilimanjaro ambayo ni mdhamini mkuu wa
mashindano hayo Pamela Kikuli, alisema kwa
miaka 13 sasa wamekuwa wakidhamini mashindano hayo, ambapo mwaka huu wametenga kiasi cha shilingi milioni 20, kwa washindi 10 wa
mbio ndefu za kilometa 42, ambapo washindi wa kike na wa kiume kwa mshindi wa kwanza
atajinyakulia kitita cha shilingi milioni nne na mshindi wa pili atanyakua shilingi milioni mbili huku mshindi watatu kwa upande wa wanaume na wanawake wataondoka na shilingi milioni moja kila mmoja.
No comments:
Post a Comment