KILIMANJARO mbunge wa Moshi mjini, Philemon
Ndesamburo (CHADEMA), ametoa kauli inayokinzani na viongozi wa UKAWA, kwa
kulitaka Jeshi la Polisi nchini liendelee kufanya kazi yake ya kuwapiga raia.
Kauli hiyo aliitoa leo ofisini kwake Mjini Moshi, alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari, ambapo alisema kuwa, haoni sababu ya
viongozi wa Ukawa kuwalaumi Jeshi la Polisi kwa kuwapiga raia.
Ndesamburo alisema kuwa, kwa sasa
wananchi wanahitaji mabadiliko, huku Jeshi la Polisi nalo likiwa limechoka,
hivyo limekuwa likifanya ukatili wa kuwapiga raia ili kuwapa hasira na Serikali
yao, na kufanya mabadiliko.
“Kitendo cha Jeshi la
Polisi kuwapiga wananchi, ni kitendo cha kuwafanya wawape hasira na Serikali
iliyopo madarakani, na kuamua kufanya mabadiliko, hivyo viongozi wa UKAWA
tunapaswa kuwaunga mkono Jeshi letu la polisi, kwani linasaidia vyama vya
upinzani kuing'oa CCM” alisema Ndesamburo.
Alisema Vyama vya upinzani vimekuwa
vikitumia siasa ya ustaarabu kwa muda mrefu bila ya mabadiliko yoyote, huku
viongozi wa CCM wakiwa wanawanyanyasa wananchi, sasa imefika wakati ambapo
mabadiliko yanahitajika.
Katika kikao cha Bunge
kilichofanyika juzi, baadhi ya wabunge wa vyama vya upinzani, wanaounda UKAWA,
walilaumu kitendo cha Jeshi la Polisi nchini, kuwapiga raia wasio kuwa na
hatia.
Sakata hili la Jeshi la Polisi
kupiga raia, lilifika bungeni baada ya kupigwa na kudhalilishwa kwa Mwenyekiti
wa chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba na wafuasi wengine wa chama
hicho.
Katika sakata hilo, wabunge wa
vyama vya Upinzani, walitaka awajibishwe Waziri mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,
Inspekta Jenerali (IGP), Ernest Mangu, Naibu wake (DIGP), Abdukrahman Kaniki,
pamoja na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa jeshi hilo, Paul Chagonja.
Wabunge wa kambi ya Upinzani
Bungeni, walitoa hoja kwa nyakati tofauti, wakati wakichangia mjadala kuhusu
hoja iliyohusu jambo la dharura, iliyotolewa na Mbunge wa kuteuliwa (NCCR-
Mageuzi), James Mbatia, na kauli ya Serikali kuhusiana na yaliyotokea Januari
27, mwaka hu, Mbagala jijini Dar es salaam.
Na Queen Isack
No comments:
Post a Comment