KILIMANJARO serikali imewaonya viongozi wa ngazi za vijiji wilayani Hai
mkoani Kilimanjaro kuacha tabia ya kuendeleza migogoro ya ardhi inayoendelea
kushamiri wilayani humo badala yake watumie nafasi walizonazo kuitatua ili
kuepusha vurugu zisizo za lazima kwa wananchi.
Rai hiyo ilitolewa na Mkuu wa wilaya ya Hai, Novatus Makunga,
wakati akizungumza na wananchi kwenye
mkutano wa kawaida wa kuwaingiza kazini wenyeviti wapya wa vitongoji waliochaguliwa hivi karibuni kwenye uchaguzi
wa serikali za mitaa katika kijiji cha Foo wilayani humo.
Makunga alisema kumekuwa na baadhi ya viongozi katika ngazi
mbalimbali za vijiji ambao huchochea migogoro ya ardhi ambayo haina tija wala
maslahi kwa serikali bali imekuwa ikigharimu maisha ya watu na kwamba nivema
sasa viongozi hao wakalenga kuitatua zaidi.
Aidha Makunga aliwataka viongozi hao kusimamia na kutekeleza
dhana ya utawala bora ili kuleta ushirikiano baina ya wananchi na viongozi wao,
ikiwa ni pamoja na kuweka itikadi za kisasa pembeni ili kufanyakazi ya
kuwatumikia wananchi kwa ufanisi zaidi.
Aliendelea kusema kuwa
ni vema viongozi na wananchi kuwa na tabia ya kusimamia miradi na shughuli
mbalimbali za maendeleo katika maeneo yao ili kuthibiti baadhi ya watu wenyenia mbaya ya kuchakachua miradi hiyo.
Alisema wenyeviti wa vijiji na vitongoji wamekuwa wakisuasua
kusimamia miradi ya maendeleo ya vijana katika maeneo yao jambo ambalo
limesababisha kuwepo kwa wingi wa vijana kuzuruza na kukaa vijiweni kutokana na
kukosa kazi za kufanya huku kukiwa na
frusa nyingi za kuwakomboa kiuchumi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Foo Judica Mmasi,
alisema kijiji hicho kimekuwa kikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ubovu
miundombinu ya barabara jambo ambalo
limekuwa likisababisha kutopitika kirahisi wakati wananchi wakiende kufuata
huduma muhimu kama afya.
No comments:
Post a Comment