Kilimanjaro kiasi
cha Shilingi bilioni 2 kimetumika kukamilisha ujenzi wa barabara katika vijiji
vya Mamba Myamba na Mpinji vilivyopo
katika Jimbo la Same Mashariki mkoani Kilimanjaro huku wananchi wa kipongeza
hatua hiyo.
Wakizungumza na mwanaharakati wa mtandao huu wa Kilimanjaro Official Blog,
wamesema tangu nchi ipate Uhuru mwaka 1961 walikuwa wakiteseka kutokana na
kukosekana kwa huduma mbalimbali ikiwemo miundombinu ya barabara.
Mmoja
wa wakazi wa Mamba Myamba, Elieti Kikoro alisema walikuwa wakilazimika kubeba
mizigo yao kichwani au kwa kutumia wanyama kama punda kutokana na miundombinu
ya barabara kuwa mibovu hususani kipindi cha masika.
Alisema
kujengwa kwa barabara hizo kumekuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi waishio
milimani katika jimbo hilo ambalo hawakutegemea kama siku moja watakuwa na
barabara ambayo itawezesha kusafirisha mazao yao.
Diwani
wa Kata ya Mamba Myamba, Michael Chikira alisema kukamilika kwa barabara hiyo
kutasaidia kufungua fursa za kiuchumi na wananchi wataweza kuzalisha kwa wingi
zao lao la tangawizi na kuinua pato la taifa. Alisema
barabara hiyo ilianza kujengwa kufuatia ombi lililotolewa kwa Rais Kikwete na
Mbunge wa jimbo la Same Mashariki Anne Kilango Malecela, ambao Rais Kikwete aliahidi
kutekeleza ombi hilo.
Kwa
upande wake Mbunge wa Jimbo hilo, Anne Kilango Malecela, alisema kujengwa kwa
barabara hizo ni msaada mkubwa kwa wananchi waishio maeneo ya milimani katika
jimbo hilo. Aidha
Kilango aliongeza kuwa barabara hizo zenye urefu wa Kilometa 13.8,
zimegharimu kiasi cha shilingi bilioni mbili, na kwamba maeneo
zilizopojengwa barabara hizo ni barabara ya Parame Kitubwa-Korogwe Mpinji (Km
8.7), na Kiwandani Manga-Chalinze (Km 4.8).
No comments:
Post a Comment