KILIMANJARO binti mwenye ulemavu wa akili anaye kadiriwa kuwa na umri
kati ya miaka kumi na tano na kumi na sita amegundulika kuwa akifungiwa kwenye shina la mgomba na
kisha kamba kufungwa kwenye mti uliopo karibu kwa muda wa miaka 10.
Tukio hili litokea katika
kijiji cha Narumu Tela wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ambapo timu ya
dawati la jinsia na watoto wiliya ya Hai walipo kwenda kijijini hapa kwa lengo
la kuitembelea familia ya mwanamke mmoja aliyefanyiwa ukatili wa kijinsia.
Kwa mujibu wa baba mdogo wa binti huyo Mr.
Korenti Willium Ngowi(37) mkulima na mkazi
wa Narumu Tela, wazazi wa binti huyo walitengana wakiwa wadogo yeye na dada
yake kabla baba yao hajafariki walikuwa chini ya uangalizi wa bibi yao Antonia
Willium Ngowi aliwalea na baba yao Beatus Willium Ngowi alipofariki waliendelea kulelewa na bibi huyo.
Ngowi anasema kuwa baada ya muda binti huyo aliugua degedege
akiwa katika umri mdogo hivyo alikuwa na tabia ya kukimbia nyumbani ndio bibi
huyo akanza kumficha na baadae kuanza
kumfungia katika shina la mgomba na kamba kufungiwa katika mti uliopo karibu na
mgomba huo.
Usiku alikuwa anawekwa katika zizi la ng`ombe analala huko
na asubui anatolewa na kufungiwa katika shina hiyo kila siku ndiyo yalikuwa maisha yake na bibi yake
akiendelea na shunguli zake za kila siku alisema Ngowi.
Anasema kuwa kwa sasa
jukumu la kumuhudumia mtoto huyo na familia nzima limeachwa kwa mdogo wao wa
mwisho Protesi Willium Ngowi anaye ishi kijiji cha Orori Narumu huwa anakuja
asubui kulisha ng`ombe na kumfungua
binti huyo kutoka kwenye zizi hilo na
kuendelea kumfunga katika shina.
Alisema Majukumu yote yameachwa kwa Protesi kwani bibi ya
binti huyo kwa sasa yupo dar es salaam kuhudhuria harusi ya mmoja wa wajukuu zake.
Binti huyo kwa muda wote amekuwa hawasiliani na mtu yeyote
isipokuwa wanafamilia wanaomhudumia ambapo
kutokana na hali hiyo amekuwa hawezi kumtazama mtu yeyeto usoni anaficha
uso wake.
Pembeni ya binti alipokuwa amefungwa palikua na vyakula vya
siku zilizopita ikiashiria kwamba hakuna mtu wa kumwangalia kama amekula au la,
na pia palikuwa na chungu.
Kwa mujibu wa majirani walisema kuwa chungu hicho huwekwa
pembeni ya binti huyo kila siku akipelekwa ndani na chungu hicho pia hupelekwa
ndani.
Binti huyo ambaye alikuwa haongei kwa kuogopa watu kwa sasa yuko chini ya uangalizi wa
polisi na baba yake mdogo Mr. Korenti Willium Ngowi ameshikiliwa na polisi huku wakisubiria
bibi huyo kurudi kutoka safarini.
No comments:
Post a Comment