KILIMANJARO mahakama ya hakimu mkazi mjini Moshi imejipanga kuanza kusikiliza kesi dhidi ya
mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Shabaan Mtarimbe na wafanyabiashara wa
mananasi mapema 23 febuari mwaka huu.
Uamuzi
huo wa kusikilizwa umepatikana baada ya mwanasheria wa upande wa
mlalamikiwa Silivia Shayo, kuomba hahakama hiyo kutoa nafasi ya
upande huo kusikilizwa .
Alisema,
haki ya kujieleza na kusikilizwa kwa pande zote mbili ni haki ya kila mtanzania
na ni democrasia ya kweli, hivyo ameitaka mahakama kutoa nafasi ya manispaa
hiyo kujitetea kabla ya hukumu.
“Kesi
hii ilisikilizwa upande mmoja tu, hivyo tunaiomba mahakama hii tukufu kutupa
nafasi ya kujieleza kabla ya kutoa uamuzi mdogo wa mahakama”
Naye
mwanasheria wa serekali David Shilatu, alisema, “Mahakama
hii tukufu, lazima iangalie hali ya wafanyabiashara hao wadogo wanaoteseka na
kutaabika kutokana na mali zilizotiwa mbaroni kuwa ndio tegemeo la familia zao
na ndizo zinazosaidia maisha ya kila
siku pamoja na familia zao.
Nae
hakiimu Julieth Mahole alihairisha kesi hiyoo hadi Februari 23 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment