Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, February 12, 2015

Wakazi wa halmashauri ya Hai mkoani Kilimanjaro washauriwa kujifunza jinsi ya kuhifadhi maji

KILIMANJARO wakazi wa halmashauri ya Hai Mkoani Kilimanjaro wameshauriwa kuanza kujifunza namna ya kuhifadhi maji safi kwenye matangi na vyombo mbalimbali vya ziada nyumbani kama njia ya kukabiliana na tatizo la uhaba wa maji lililoanza kujitokeza hivi karibuni, hasa kwa wakazi wa Hai mjini na mitaa yake.

Ushauri huo umetolewa leo na Enginia Prosper Shoo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu tatizo la upungufu wa maji ulioanza kujitokeza wilayani Hai.

Shoo alisema kuwa kiwango cha maji kinachozalishwa kimeshindwa kutosheleza mahitaji ya wakazi wote kwa siku kutokana na kiangazi, uharibifu wa mazingira, ongezeko la matumizi ya maji, kwani mradi huu ulianzishwa mwaka 1990 kwa lengo la kuhudumia watu elfu 64, lakini kwa sasa watumiaji wameongezeka hadi kufikia watu zaidi ya laki moja.

''Natumia fursa hii kuwaarifu wakazi na wateja wetu kwamba matumizi ya maji safi yamekuwa makubwa na hayalingani na uwezo, haya maji yaliletwa kwa ajili ya binadamu kuyatumia kwa matumizi madogo madogo na sio kwa ajili ya ujenzi, umwagiliaji na uoshaji wa magari.

Nawaomba wananchi watumie maji kwa uangifu kwa kipindi chote kwa sababu huduma sasa inatolewa kwa mgao maalumu, pia imegundulika wateja wengi wamejenga visima vya maji chini ambavyo wanafungulia maji muda wote ili kujiwekea akiba, hii inaharibu mtandao mzima wa mtiririko wa maji na matanki kutoweza kuhifadhi maji wakati wa usiku.

Shoo alisema hivi sasa ofisi yake inatafuta fedha kiasi cha bilion 7.8 ili kuweza kumaliza tatizo hilo, tumepeleka maombi yetu wizara ya maji na kwamba bodi haina uwezo.

No comments:

Post a Comment