Kulia ni Kajo akiwa na King Jofa wa Kilimanjaro Official Blog.
Baadhi ya bloggers waliohudhouria katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyokutanisha bloggers
kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wakifurahia sherehe yao.
Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyokutanisha bloggers kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.
Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyokutanisha bloggers kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.
Baraza
la Habari Tanzania (MCT) limekubali kuanza ushirikiano na uhusiano
mzuri na Chama cha Bloggers Tanzania (TBN) mara kitakapo maliza mchakato
wa usajili wake na kutambulika rasmi kisheria. MCT imesema kwa hatua ya
kwanza itafanya mazungumzo na viongozi wa TBN na kujadiliana namna gani
ya kuisaidia TBN.
Kauli
hiyo imetolewa juzi jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa MCT,
Kajubi Mkajanga alipokuwa akizindiwa hafla ya kwanza ya mwaka 2015 ya
wamiliki na waendeshaji wa blogu na mitandao mingine ya kijamii
iliyofanyika katika Hoteli ya Serena.
Katibu
huyo Mtendaji wa MCT alisema kwa maendeleo ya sasa ya teknolijia ya
habari na mawasiliano ni vigumu kuzitenga blogu kama vyombo vya habari,
hivyo kuahidi kushirikiana na TBN kuhakikisha inafikia malengo yake ya
kuwaunganisha bloggers na kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili.
Alisema
MCT inasubiri TBN ipate usajili kisheria toka mamlaka husika serikalini
na baada ya zoezi hilo itaanza kushirikiana maramoja na chombo hicho
kilichoanzishwa kuwaunganisha wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya
kijamii nchini na wale wanaofanya shughuli za nje ya nchi.
“…MCT
ipo tayari wakati wowote kuanza kushirikiana nanyi kikazi,
tunachosubiri ni TBN kusajiliwa rasmi…mtakapo maliza usajili tu njooni
ofisi, tutazungumza na viongozi wenu ili kujua nini cha kuwasaidia.
Naombeni msichelewe tuanze hili mara moja,” alisema Kajubi Mkajanga
akizungumza na wana-TBN kabla ya kuzinduwa sherehe hiyo.
Awali
akizungumza katika hafla hiyo Mwenyekiti wa TBN, Joachim Mushi alisema
kwa sasa mitandao ya kijamii imekuwa ikitekemewa na kundi kubwa la jamii
katika kusambaza taarifa kwa haraka licha ya uwepo wa changamoto kadhaa
ndani ya tasnia hiyo.
Alisema
pamoja na mambo mengine, TBN imeanzishwa kwa lengo la kuwaunganisha
waendeshaji na wamiliki wa blogu pamoja na mitandao mingine ya kijamii,
na pia kuhakikisha wana-TBN wanapata fursa ya kujifunza zaidi maadili ya
tasnia ya habari na mawasiliano ili kufanya kazi zao kiufanisi zaidi.
Aidha aliishukuru Kampuni ya Simu ya
Vodacom Tanzania kwa kusaidia kufanikisha tukio la kukutana ‘bloggers’,
pamoja na Benki ya NMB na makampuni mengine ya Coca Cola, AIM Group na
kampuni ya huduma za intanenti ya Raha kufanikisha tukio hilo la
kuwaleta pamoja bloggers wa Tanzania.
Akisoma risala ya wana-TBN kwa mgeni
rasmi, Mjumbe wa TBN, Henry Mdimu alisema licha ya blogu kuwa chanzo
kikubwa cha habari na mstari wa mbele kuwafikishia wananchi habari kwa
haraka zaidi lakini bado zimekuwa hazitambuliwi na mamlaka zinazosimamia
na kutetea tasnia nzima ya habari.
“…Pamoja na kazi kubwa na nzuri
inayofanywa na ‘bloggers’ na waendeshaji wa mitandao ya kijamii, bado
hawatambuliki rasmi na mamlaka husika pamoja na taasisi zinazohusika na
usimamizi wa tasnia hii likiwemo Baraza la Habari Tanzania (MCT), Idara
ya Habari (Maelezo), MISA-Tan na hata Mfuko wa Ruzuku kwa Vyombo vya
Habari nchini (TMF).
“..Tunasema hivi maana tunaona kwa
namna moja ama ingine wadau hawa muhimu hawajumuishwi katika harakati au
michakato yoyote ile mnayoifanya kwenye tasnia hii. Mfano kupata semina
za MCT, kupewa vitambulisho (Press card), kushiriki katika mafunzo na
hata mashindano ya kila mwaka ya wanahabari yanayoandaliwa na MCT,”
alisema Mdimu akisoma risala ya TBN mbele ya mgeni rasmi Bw. Mkajanga.
Kwa
upande wa waalikwa rasmi kutoka ubalozi wa Marekani wakizungumza katika
hafla hiyo kupitia kwa mwakilishi wao ameahidi kuisaidia TBN katika
programu mbalimbali ili kuchochea uhuru wa habari nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment