Kikosi cha Simba Sport Club
Kikosi chaYoung Africans Sports Club
Mechi no.117 iliyowakutanisha Simba na Yanga katika uwanja
wa Taifa, imeingiza jumla ya sh. milioni 436,756,000 kutokana na idadi ya watazamaji
49,758 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.
Watazamaji 309 walikata tiketi za VIP A, 1,310 VIP B, 1,533
VIP C, Rangi ya Machungwa (Orange) 9,913 huku viti vya rangi ya bluu na kijani
wakiingia watazamaji 36,693.
Mgawanyo wa mapato ya mchezo huo ni VAT 18% sh.66,623.796,
FDF timu mwenyeji sh. 17,415,300, FDF TFF sh.7,463,700, Gharama za tiketi
sh.11,669,600.
Mgao wa Uwanja sh. 50,037,540.51, Gharama za mchezo
sh.28,354,606.29, Bodi ya Ligi (TPLB) sh. 26,686,688.27, TFF sh.20,015,016.20,
DRFA sh. 11,675,426.12, klabu ya Simba sh. 115,086,343 huku Yanga wakipata
sh.81,727.83.
Wakati huo huo Ligi Kuu ya Vodacom itaendelea kesho siku ya
jumanne katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, wenyeji timu ya Polisi Morogoro
watawakaribisha Ruvu Shooting kutoka Mlandizi mkoani Pwani.
Siku ya jumatano JKT Ruvu watawakaribisha Young Africans
katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku jijini Tanga Mgambo Shooting
wakiwa wenyeji wa timu ya Azam FC.
Chanzo: Umojahabari Blog
No comments:
Post a Comment