DODOMA Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Dodoma Mjini kimefanikiwa kufungua matawi 10 ya msingi ya chama hicho yenye wanachama zaidi ya 3,500 ambao ni waendesha pikipiki maarufu bodaboda.
Akizungumza na kituo hili mjini Dodoma katibu Mwenezi wa wilaya ya Dodoma mjini Juma Mtaalam baada ya kuzindua tawi la waendesha bodaboda lililopo CBE amesema kuwa kwa sasa vijana wameamka na kupania kiadhibu CCM kupitia sanduku la kura.
Mbali na hilo Mtaalam amesema kuwa wilaya ya Dodoma mjini imeweka mikakati ya utoaji elimu ya uraia na kujitambua kwa vijana huku akisema kuwa kauli mbiu ni Dodoma bila CCM imawezekana.
Naye mwenyekiti wa baraza la wanawake Chadema wilaya(BAWACHA)Hadja Maula,aliwataka akina mama kuachana na ushabiki wa kuishabikia CCM kwani CCM indicho chama ambacho kinawasabishia kujifungulia chini ya miti.
Amesema kuwa matatizo mengi ambayo yanawakumba akina mama wajawazito pamoja na watoto chini ya miaka 5 yanasababishwa na udhaifu wa viongozi wa serikali ya CCM.
Kwa upande wake Josehine Kihoza ambaye ni mtangaza nia ya ubunge jimbo la Dodoma mjini kupitia chadema amesema kuwa mkoa wa Dodoma unatakiwa kuwa na mabadiliko ya kweli ambayo yanatokana na Chadema kwa kushirikiana na umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA).
Mtangaza nia huyo amesema kuwa kwa miaka zaidi ya 54 ya uhuru Dodoma haikuweza kuongozwa na vyama vya upinzani lakini kwa sasa wameamka na kutaka Dodoma kuwa mkoa wa mabadiliko tofauti na ilivyo sasa.
No comments:
Post a Comment