Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, April 2, 2015

Fahamu jinsi pombe za kienyeji zinavyowapa wanawake nguvu ya kuwapiga wanaume



KILIMANJARO imekua kama desturi kwa wanawake na wanaume katika swala la unywaji wa pombe za kienyeji katika kijiji cha Kingereka A, kata ya Hai Mjini, Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, imepelekea hali ya ulinzi kwa mama na mtoto kuwa hatarini kutokana na ulevi ulio kithiri.

Hayo yalisemwa jana na katibu wa timu ya ulinzi wa mama na mtoto  Kingereka, Bibi Rustina Tarimo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake  juu ya masuala ya ulinzi wa mama na mtoto.

Alisema kuwa kumekuwa na tabia ya unywaji wa pombe za kienyeji kwa Wanaume na Wanawake ndani ya eneo hilo hali ambayo inapelekea migogoro na ukatili  wa kifamilia hasa kwa mama na watoto.

Alisema suala la wanawake kunywa pombe muda wa kazi na mapumziko kupita kiasi  ni hatari kwa jamii ya sasa kutokana na watoto kuachwa nyumbani bila uangalizi wa wazazi wote wawili pamoja na kuachwa pasipo chakula jambo ambalo ni kinyume na malezi.

Alisema mbali na hayo baadhi ya wanawake wamekuwa wakipiga waume zao mara baada ya kunywa pombe za kienyeji hali ambayo haileti usawa katika ngazi ya familia kwani migogoro kama hiyo inachangiwa na unywaji wa pombe kupindukia.

Kwa upande wake mwanaharakati wa haki za binadamu toka shirika lisilokuwa la kiserikali la Lady Circle Kilimanjaro, Messe Ndosi alisema kuwa hali hiyo ya ulevi wa kupindukia unapelekea matatizo mengi kujitokeza katika jamii hali ambayo isipo dhibitiwa itapelekea migogoro na ukatili kuongezeka.

“Kwa kweli naweza nikasema kuwa baadhi ya wanawake wanatumia uwezo wa kifedha labda aliyo ipata kupitia mikopo kutumia fedha hizo kunyanyasa wanaume zao kwa kunywa pombe kupita kiasi na kuwashushia kipigo waume zao” Alisema Ndosi.

Ametoa wito kwa jamii ya wakaazi wa Wilaya ya Hai kutoa ripoti kwa timu ya ulinzi wa mama na mtoto katika maeneo yao, ustawi wa jamii na  Dawati la Jinsia na watoto kuhusu matukio ya ukatili yanayotendeka katika jamii zao ili ukatili uweze kupigwa vita na kujenga jamii yenye usawa na pia kumrudia Mungu.

No comments:

Post a Comment