Orodha ya majina ya maafisa wakuu wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi imewasilishwa katika mabunge mawili nchini Kenya huku kukiwa na mjadala mkali kuhusu jinsi orodha hiyo ilivyowasilishwa bungeni.
Kikao cha bunge la senate lilisitishwa kwa muda kuruhusu wabunge kusoma ripoti hiyo. Katika
bunge la taifa wabunge nao walitaka kuzima mjadala kuhusiana na ripoti
hiyo iliyowasilisha na raia kwa misingi ya kukiuka sheria.
Robert Kiptoo ana maelezo zaidi kutoka Nairobi.
"Orodha
hiyo ina majina 175 ya maafisa wakuu serikalini wakiwemo mawaziri,
makatibu wa wizara na maafisa wengine wa taasisi za umma na hata za
kibinfasi."
Maafisa hao wa serikali sasa wameshurutishwa kungatuka madarakani kwa muda wa siku sitini ili kuruhusu uchunguzi wa kina. Orodha
hiyo ambayo wakenya wakisubiri kwa kwa hamu na ghamu hatimaye
ilijadiliwa katika mabunge yote licha ya upinzani kutoka kwa wabunge
kadhaa.
Mjadala mkali uliibuka katika mabunge hayo hadi spika wa
bunge la senate kusitisha kikao kwa muda kuruhusu masenate kusoma ripoti
hiyo ya rais. Hata hivyo mjadala ulipoanza wabunge wengi
wanaoegemea upande wa serikali waliunga mkono wakisema vita dhidi ya
ufisadi ni sharti viimarishwe.
wabunge wa upinzani nao wakijaribu kupinga mjadala huo, wakidai kuwa sheria haikufuatwa na rais alipowasilisha ripoti hiyo.
Aidha wamesema kuwa ripotio haina sahihi kama inavyohitajika.
Mpinzani
mkuu wa rais Kenyatta na kiongozi wa upinzai, Raila Odinga, akiongea
baada ya kuwasili nchini kenya kutoka uchina siku ya jumapili, alisema hatua hiyo ya rais ni sawa na ulaghahi dhidi ya wakenya.
Amesema
kutoka na jinsi mfumo wa mahakama upo, ni vigumu sana kwa uchunguzi
dhidi ya maafisa 175 kukamilishwa kwa siku sitini ikizingatiwa kuwa kuna baadhi ya kesi za ufisadi ambazo zimesalia mahakamani kwa zaidi ya miaka kumi.
Mjadala
kuhusu ripoti hiyo ya rais inarajiwa kuendelea kwa muda wa siku tatu
zijazo huku wale waliotajwa wakihitajika kungatuka madarakani hadi
uchunguzi utakapokamilika.
Chanzo: BBC Swahili
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment