Baadhi ya Viongozi wa makanisa wilayani siha mkoani kilimanjaro wametakiwa kuacha tabia ya kujiingiza katika migogoro ya kisiasa na badala yake waungane kwa pamoja kuleta upatanishi na kudumisha amani iliyopo katika nchi hii ya Tanzania.
Kauli hiyo ilmetolewa jana na Mchungaji Josephat Massawe wa Kanisa la Pentekost lililopo Magadini Sanya juu Wilayani siha mkoani kilimanjaro wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu msimamo wa kanisa hilo katika suala la katiba iliyopendekezwa.
Kauli ya mchungaji huyo inakuja baada ya kuibuka kwa mgogoro baina ya Askofu mkuu wa kanisa katoliki mwadhamu Polycarp Kardinal Pengo na mchungaji kiongozi wa kanisa la ufufuo na uzima Josephat Gwajima, kuhusu katiba iliyopendekezwa.
Mchungaji huyo alisema kuwa kutokana na hali hiyo yeye na kanisa hilo msimamo wao ni kwende kuipigia kura katiba iliyopendekezwa na sio vinginevyo kutokana na umuhimu wake.
Alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi wote kujitokeza na kuipigia kura katiba hiyo kwani wasipokwenda mwisho wa siku hakuna wakumlaumu na kwamba zaidi ya hapa watakuwa wamepoteza haki zao za msingi.
Akizungumzia kuhusu maneno ya Kardinal Pengo juu ya katibu hiyo, Mchungaji Josephat Massawe alisema "Pengo hakufanya jambo baya kwani maneno aliyoyatoa yalikuwa ni mawazo yake hivyo kila mmoja anapaswa kuyapima kabla ya kutoa maamuzi"
No comments:
Post a Comment