Kauli hiyo imetolewa na kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Bahi, Stuart Kiondo, wakati akitoa elimu kwa wafugaji juu ya madhara ya kutoa na kupokea rushwa.
Akizungumza na wafugaji hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Chali Isanga kata ya Chipanga Wilayani Bahi, amesema kuwa taasisi hiyo imelazimika kutoa elimu hiyo ili kila mfugaji aweze kuelewa kutambua madhara ya kutoa au kupokea rushwa.
Aidha kamanda huyo amesema kuwa iwapo wafugaji wataendelea kutoa rushwa kwa viongozi wao ni wazi kuwa hawatatendewa haki kwani rushwa hupotosha ukweli na ni adui wa haki.
Kamanda huyo amesema kuwa kwa kuwa wafugaji wamejiwekea utaratibu wa kulipia michango mbalimbali kupitia mifugo waliyonayo kama vile ng’ombe na punda kila mmoja utozwa sh.1000 wakati mbuzi,kondoa na nguruwe utozwa sh 500 kila mmoja hivyo ni vyema utaratibu huo ukafuatwa.
Akizungumzia kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu amewataka watanzania kutokukubali kupewa rushwa ili kumchagua kiongozi fulani bali wamchague kiongozi mwenye sifa ya kulinda maslahi ya taifa kwa ujumla.
Naye Said Nyambaa ambaye ni mfugaji wa eneo hilo ameiomba TAKUKURU kufika mara kwa mara kutoa elimu kwa jamii hiyo pamoja na maeneo mengine ili kukabiliana na rushwa katika Taifa la Tanzania.
No comments:
Post a Comment