Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Makundi ya Watu wenye Ulemavu waliokataa tamaa (TASODEFA) mkoani Dodoma,Paul Mahanyika alipokuwa akizungumza na kituo hiki mjini Dodoma.
Amesema wanasiasa wamekuwa wakitumia udhahifu wa watu wenye ulemavu kutokana na hali ngumu ya kimaisha waliyokuwanayo kwa kuwapatia fedha na zawadi kama kishawishi cha kutaka wawachague kwenye uchaguzi utakaofanyika mwaka huu.
Bwana Mahanyika pia ameishauri jamii ya watu wenye ulemavu kuwaepuka viongozi watakaojitokeza na kuonyesha dalili za kuomba kura kwa kutaka kuchaguliwa kwa kuwashawishi kupewa fedha na zawadi,wajiepushe na wanasiasa hao kwa kuwa kufanya hivyo watakuwa wameuza thamani ya utu na haki yao ya kimsingi ya kumchagua kiongozi wanaemtaka.
Pia ameitaka jamii inayoishi na watu wenye ulemavu kutowageuza walemavu hao kama sehemu yao ya kujipatia fedha kutoka kwa wanasiasa kwa lengo la kuwashawishi ili wawapigie kura ya ndiyo pindi uchaguzi utakapowadia wa ngazi ya udiwani,ubunge na urais.
Amesema kutokana na ugumu wa maisha waliokuwanao karibu familia nyingi za watu wenye ulemavu baadhi ya watu wanaoishi nao wamekuwa wakiwashawishiwa wapokee fedha na zawadi toka kwa wanasiasa ili wawapatie na waweze kuwachagua katika uchaguzi.
No comments:
Post a Comment