Isanja alitoa wito huo kwenye semina ya mafunzo kwa ajili ya wakufunzi wa Vicoba iliyofanyika mjini Moshi, mkoani humo, juzi.
Amesema kuwa Vicoba imekuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wengi wakiwemo baadhi ya wanaume ambao wamejiunga navyo hivyo dhana kuwa ni vya wanawake pekee haina mashiko.
Akiongea kwenye semina hiyo, mratibu wa mtandano wa Vicoba manispaa ya Moshi, Rose Tesha, amesema kuwa wahitimu wa mafunzo hayo watakuwa na jukumu la kutoa mafunzo maeneo mbalimbali mkoani Kilimanjaro.
Rose amesema kuwa mtandao huo wa Kivinet una jumla ya wanachama 290 na kwamba wengi wa wanachama kwenye vikundi hivyo ni wanawake.
Nae Mkurugenzi mtendaji wa Kivinet Martha Mwingira, amesema moja wapo ya changamoto kubwa katika mtandao huo ni wanachama wengi kujiunga wakiwa na lengo la kufuata mikopo.
“Mikopo ni fursa na lengo moja wapo ni kumnufaisha mwanachama ni vyema wakajiepusha na tamaa za mikopo ambazo zitageuka kuwa mizigo kwao”, alionya.
No comments:
Post a Comment