Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, May 19, 2015

Asilimia kumi ya fedha kwaajili ya vijana na akina mama bado ni changamoto kubwa

Meya wa Manispaa ya Moshi Jafari Michael.

KILIMANJARO: Meya wa Manispaa ya Moshi Jafari Michael, ameeleza kuwa utekelezaji wa kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya mfuko wa vijana na wanawake imekuwa ngumu kutekelezwa kutokana na ucheleweshewa fedha za kujiendesha kwenye Halmashauri hivyo kujikuta zikitumia mapato ya ndani na kukosa fedha kwa wakati kwa makundi hayo.

Meya alibainisha hayo wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wanafunzi waliohitimu mafunzo mbalimbali ikiwemo ya ujasiriamali kwa mwaka mmoja yaliyotolewa na Kanisa la Tanzania Assembles Of God (ICC), Moshi.

Alisema kuwa licha ya kuwepo kwa fedha ambazo hutakiwa kutengwa kutoka kwenye mapato ya ndani kwa ajili ya vijana na akina mama bado zimekuwa zikichukua muda mrefu kutolewa kwa wahusika kutokana na fedha zinazopatikana kwenye Halmashauri kuingia kwenye matumizi mengine.

Akitolea mfano kwa Manispaa ya Moshi, Alisema kuwa mwaka 2014/15 milioni 282 zilitengwa kwa ajili ya vijana na akina mama lakini mpaka sasa ni kiasi cha shilingi millioni 40 pekee zimetolewa kwa kundi hilo kupitia VICOBA pamoja na SACCOS.

Alisema kwa sasa halimashauri hiyo inafikiria kutenga shilingi milioni themenini (80,000,000) kwa ajili ya vikoba na kwamba ndani ya vikoba ndiko kuliko vijana na kina mama ambao ndio walengwa wa fedha hizo.

Mchungaji wa Kanisa la ICC, Glorious Shoo alisema wasichana waliopatiwa mafunzo hayo walichukuliwa katika mazingira magumu na hatarishi, ambapo kati ya wasichana 10 walioanza mafunzo hayo nusu yao walikuwa wameshaambukiwa virusi vya UKIMWI.

Hata hivyo alisema kuwa licha ya wasichana hao kuwekwa kambini na kugaramikiwa mahitaji yote muhimu pamoja na mafunzo wawili pekee ndo waliweza kuhitimu mafunzo hayo ya mwaka mmoja huku wengine wakiacha kutokana na sababu mbalimbali.

Alisema tangu kuanza utaratibu huo, wamegundua sababu mbalimbali ambazo zimekuwa zikipelekea wasichana wengi kujiingiza katika makundi maovu ikiwemo kuuza miili yao kuwa inatokana na mazingira magumu pamoja na kukosa elimu.

No comments:

Post a Comment