Mh. Davis Mosha akizungumza na wakazi wa Moshi katika Mkutano wa Kuwaaga. |
Aliyekua Mgombea Ubunge Jimbo la Moshi Mjini kupitia tiketi
ya Chama cha Mapinduzi Mh. Davis Elisa Mosha amewaaga Wananchi na wanachama wa
ccm jana jioni katika vbiwanja vya Penfold vilivyopo katika hifadhi ya Raylway
Mjini Moshi. Katika Mkutano huo uliohudhuriwa na Mamia ya Wananchi wa Moshi
huku wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakiwa wamevalia Nguo za ccm.
Baada ya viongozi mbalimbali kumaliza kuongea ndipo majira
ya saa kumi na Moja Mh. Davis Elisa Mosha alipata fura ya kuzungumza na Wananchi
wa Moshi na kuwaaga. Kitendo cha Mosha kupanda jukwaani kulizua kelele na
shangwe kwa Wananchi zilizodumu kwa Zaidi ya dakika tano mpaka pale alipowaomba
wamsikilize. Mosha alianza kushukuru Wananchi wa Moshi kwa upendo mkubwa
waliomuonesha katika kipindi chote cha Miezi mitatu aliyokaa nao Pamoja katika
harakati za kuomba ridhaa ya kuongoza jimbo la Moshi na kuleta Maendeleo.
Sehemu ya Umati wa wananchi wa Moshi waliojitokeza kumsikiliza Mh. Davis Mosha. |
Pia Mosha aliweza kuwalaumu viongozi wa ccm kwa kushiriki
katika harakati za kudhoofisha jitihada zake za kuongoza jimbo hili huku
akiwaasa wanachama wa ccm kutumia nafasi iliyopo kuweza kubadili uongozi wa
chama kama kweli wana nia ya dhati ccm ije kuongoza jimbo la Moshi Mjini.
“Baadhi ya viongozi wa ccm wamenunuliwa, Ni mamluki na
wanakiuza chama. Si wakati wa kulia Wananchi wa Moshi na wanachama ni wakati wa
kuanza kwa mchakato wa kusafisha chama ndani ya Moshi na kuwaondoa viongozi
ambao si waaminifu” Alisema Mosha.
Wananchi wakiwa hawaamini kama Mh. Davis Mosha ndio anawaaga sasa. |
Hata hivyo hali ilibadilika Ghafla baada ya Davis Mosha
kutangaza kutorudi na kugombea tena ndani ya Jimbo la Moshi ndipo Wananchi na
wanachama walipoangua kilio na wengine kuzimia. Hali hiyo ililipa kazi ngumu
jeshi la Polisi kwa kuwa hawakua wamejiandaa na hali iliyojitokeza pamoja na
kutokuwepo na watu wa huduma ya Kwanza. Kitendo hicho kilipelekea viongozi
mbalimbali wa ccm na Wananchi kumuomba Mosha kusitisha maamuzi yake ili
kunusuru Maisha ya Wananchi hao waliokua wakilia kwa uchungu na wengine
kutishia kujidhuru. Mosha aliwasihi wasilie na aliwaahidi kuimiza ahadi zake
zote alizoahidi ambazo zipo ndani ya uwezo wake.
Wananchi na wanachama wa ccm wakiangua vilio kwa majonzi. |
Mwishoni ililazimu jeshi la Polisi kumshinikiza Ndugu Mosha
kushuka jukwaani na kuelekea katika Gari lakini Wananchi walimzuia kuingia
kwenye gari na kutembea nae Zaidi ya kilometa tano kutoka eneo la Mkutano mpaka
Nyumbani kwake Kiboriloni. Baada ya kufika nyumbani Wananchi hawakuridhika
walimzuia kuingia ndani mpaka azungumze nao ndipo alipozungumza nao na
kuwaahidi hatoondoka mpaka ajue hatima ya Jimbo la Moashi ikiwemo kushughulikia
baadhi ya tuhuma za sitofahamu zinazohusu mapungufu ya Uchaguzi.
Jeshi la Polisi likimsindikiza Davis Mosha baada ya kumalizika kwa Mkutano. |
No comments:
Post a Comment