Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, November 25, 2015

AMANA BANK WAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA - ARUSHA

















Benki ya kwanza ya kiislamu Tanzania, Banki ya Amana "Amana Bank" inaadhimisha miaka minne tangu kuanza rasmi kutoa huduma zake kwa wateja mnamo 24 Novemba 2011.Wakuu wa idara Mameneja na wafanyakazi wengine wote watakuwa wakikutana na wateja na kuwapatia huduma mbalimbali kupitia matawi yao yote yaliyopo katika majiji ya Dar es salaam, Arusha na Mwanza.

Amana Bank ambayo kwa sasa ina wateja zaidi ya 20,000 na matawi 7 Tanzania nzima, inachukua fursa katika maadhimisho haya kuwashukuru wateja wake wote kwa kuwa wazalendo na kuichagua Amana Bank kama pendekezo lao kwa huduma za kibenki. Amana Bank inaahidi kuendelea kuwekeza na kukuza mtandao wake na kuleta bidhaa na huduma bora Zaidi na za kisasa.

Katika kipindi hichi maalum kwa benki ya Amana, uongozi na wafanyakazi wa Amana Bank wameahidi kushirikiana na wateja wa ndani na nje kwa kuwapatia huduma bora zaidi. Huku wakiamini wateja ndio muhimili wa mafanikio ya bank yao, lengo kubwa ni kuwaridhisha wateja wao na wamejidhatiti kuwapa huduma bora muda wote bila kujali mahali walipo.

Uongozi wa Amana Bank wameahidi kuwapatia wateja wao huduma za kiwango cha juu kwa ajili ya mahitaji yao ya binafsi au kibiashara muda wote. Maadhimisho haya yatahitimishwa ijumaa ya tarehe 27/11/2015, kwa hafla ya kuwazawadia wateja na wafanyakazi katika matawi ya Amana Bank. 

No comments:

Post a Comment