Timu ya Mpira
wa Miguu ya Mkoa wa Kilimanjaro inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania
bara ambayo imemaliza mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo ikiwa inashikilia nafasi ya
tatu katika kundi C huku kundi hilo likiongozwa na JKT Oljoro. Katika kuimarisha
timu nakuongeza nguvu timu hiyo imekuwa moja ya timu ambazo zimeshtua wapenzi wa
soka Tanzania kwa kuweza kuanza usajili na eneo muhimu katika timu huku wakihusisha
mtu muhimu maarufu na mwenye mchango mkubwa katika soka la Tanzania.
Mwenyekiti wa bodi ya Panone Alhajj Mohamed Karia akifafanua jambo kwa Minziro |
Akizungumza na
Mtandao huu Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Panone Fc Alhaji Mohamed Karia
Mara baada ya kuinyaka sahihi ya Aliyekua kocha wa JKT Ruvu Kocha Fred Felix
Minziro kutoka Dar es salaam. Akizungumza kwa furaha Alhajj Karia alisema ilikuwa
ni kazi ngumu kwao kuinyaka sahihi ya Kocha huyo kwa kuwa ni kocha mkubwa na ametoka
katika klabu ambazo zipo daraja la juu na huku wakiwa na presha ya kumkosa kocha
huyo kwa kuwa alikua akinyatiwa na club ya African sports ya Jijini Tanga lakini
tayari sasa ni kocha wetu kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Alhajj Karia akipeana mkono na Minziro baada ya kumaliza kuweka sahhi mkataba. |
“Ilitulazimu
kumchukua na kukaa nae hotelini kwa muda wa siku tano huku tukifanyanae mazungumzo
pamoja nakumpa wasaa wakuifahamu timu.Tunashukuru ameweza kuikubali timu na kuridhika
kuweza kuwavusha wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro kwa kuwapatia timu ya ligi kuu”
Alisema Alhajj Karia.
Pia Mwenyekiti huyo wa bodi alitumia wasaa huu
kuwaomba wakazi wa mkoa Kilimanjaro kuiunga mkono timu ya Panone kwanini timu ya
Mkoa wa Kilimanjaro na wasitoe mwanya wa
maneno ambayo yanaweza kukwamisha ndoto za wengi.
“Sina mengi ya
kuongea nimeshukuru kwa uongozi wa Panone kwa kuweza kuniamini na sasa naomba wapenzi
wa mpira na walimu wenzangu wa mpira tushiriki kuijenga timu ya panone fc”
Alisema Minziro. Hata hivyo alipoulizwa kuhusu usajili Minziro alisema anategemea
kuanza mechi za majaribio siku ya jumatatu nawachezaji takribani kuminasita kutoka
sehemu mbalimbali wataungana na wachezaji waliopo wa Panone na kufanya mazoezi na
mwisho ataweza kujua ni kikosi gani kitaweza kuingia kambini rasmi kwa ajili ya
mazoezi na kujiandaa na Ligi inayotarajiwa kuanza mapema disemba 26.
No comments:
Post a Comment