Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky
Sadicky akizungumza wakati wa kukabidhi Madawati 50 yaliyotolewa na
benki ya Azania tawi la Moshi kwa shule ya msingi Mnazi katika manispaa
ya Moshi ikiwa ni kuunga mkono agizo la rais John Magufuli la kupunguza
tatizo la Madawati kwa shule za msingi.
Meneja wa benki ya Azania tawi la
Moshi,Hajira Mmambe akizungungumza juu ya hatua ya benki hiyo kuunga
mkono agizo la rais John Magufuli la kutatua tatizo la Madawati kwa
shule za msingi nchini.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga
akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi Madawati 50 yaliyotolewa na
benki ya Azania tawi la Moshi kwa shule ya msingi Mnazi.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Azania tawi la Moshi wakifuatilia hafla hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Moshi,Deodatus Nyoni akizungumzia juu ya upungufu wa
Madawati 701 ulipo sasa kwa shule za msingi na Sekondari.
Meneja wa benki ya Azania tawi la Moshi,
Hajira Mmambe akimkabidhi mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky
Sadicky Madawati yaliyotolewa na benki hiyo. Wengine ni wanafunzi wa
shule ya msingi Mnazi.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky
Sadicky (katikati) akiwa ameketi kwenye moja ya Madawati yaliyotolewa na
benki ya Azania tawi la Moshi kwa shule ya msingi Mnazi, kulia ni mkuu
wa wilaya ya Moshi, Novatus Makunga na kushoto ni meneja wa Azania benki
tawi la Moshi, Hajira Mmambe.
Wanafunzi katika shule ya msingi Mnazi wakiwa wamekaa katika Madawati yaliyotolewa na benki ya Azania tawi la Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadicky, akisalimiana na wanafunzi katika shule hiyo.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi,
Raymond Mboya akitoa neno la shukrani mara baada ya kupata msaada wa
Madawati kutoka Benki ya Azania tawi la Moshi.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi,
Raymond Mboya akiteta jambo na Meneja wa benki ya Azania tawi la Moshi,
Hajira Mmambe wakati wa hafla ya kukabidhi wa Madawati kwa shule ya
msingi Mnazi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky
Sadicky akisalimiana na wafanyakazi wa benki ya Azania tawi la Moshi
pamoja na watumishi wa halmashauri ya Manispaa ya Moshi.
Na Dixon Busagaga.
No comments:
Post a Comment