Muungano wa vyama vya upinzani nchini Tanzania umeahirisha maandamano ya kitaifa ambayo yalikuwa yamepangiwa kufanyika kesho.
Viongozi wa upinzani, akiwemo Edward Lowassa wa Chadema, wametangaza hatua hiyo kwenye kikao na wanahabari Dar es Salaam.
Wamesema
wameahirisha maandamano hayo kwa kipindi cha mwezi mmoja baada ya
kusikia ombi la viongozi wa kidini na wadau wengine waliowaomba
kukumbatia na kuyapa muda mazungumzo.
Viongozi wa chama hicho
walikuwa wameitisha maandamano na mikutano ya kisiasa Septemba Mosi
kupinga walichosema kuwa ni ukandamizaji unaoendelezwa na serikali.
Baada
ya mkutano wa kikao cha Kamati Kuu ya chama Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) mwishoni mwa Julai, viongozi walisema: "Yapo Matukio
ambayo yamekua yakifanywa na kukandamiza demokrasia na misingi
ikipuuzwa na kudharauliwa."
"Si nia ya Chadema kugombana na Serikali bali ni kazi ya Chama
Pinzani kuisaidia Serikali iongoze kwa kufuata misingi ya Katiba," chama
hicho kilisema.
Maandamano hayo yalipewa jina Ukuta, ikisimamia Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania.
Serikali ilipiga marufuku mikutano yote ya kisiasa,
ya hadhara na ya ukumbini. Baadhi ya viongozi wa upinzani wamekamatwa na
kuzuiliwa kwa muda.
Chanzo: bbc Swahili
Chanzo: bbc Swahili
No comments:
Post a Comment