Pichani kati ni Mratibu wa tamasha la Dar Festival, Faridi Faradj
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), jijini Dar es
Salaam juu ya tamasha hilo litakalofanyika mwezi huu katika viwanja
vya viwanja vya leaders club na siku ya pili ndani ya viwanja vya
Makumbusho jijini Dar.Kulia ni Diwani wa Kata ya Ilala na kushoto ni
mmoja wa Waratibu wa tamasha hilo, Shaban Kapilima.
Mratibu wa Tamasha hilo ,Faridi Faradj amesema kuwa tamasha jipya litalenga kutangaza na kudumisha utamaduni wa Tanzania, na kuwa tamasha hilo litahusisha michezo ya kiasili kama Bao, Karata itayoenda sambamba na burudani nyingine za ngoma za asili na maonesho ya baadhi ya tamaduni za makabila ya Tanzania.
"Pia tunategemea kuwa na mashindano ya kucheza, vichekezo na maonesho ya Muziki kutoka kwa baadhi ya Wasanii" alisema Faridi.
Amesema kuwa kutokana na utafiti inaonesha watu wengi wamekuwa wakikosa matukio kama haya ya hivyo wanatarajia tamasha hilo litapokelewa kwa furaha kubwa na Watanzania watajitokeza kwa wingi kwani litahusisha watu wa rika mbalimbali.
Akifafanua zaidi faida ya tamasha hilo, Faridi amesema kuwa tamasha hilo litaendeleza umoja wa Watanzania, Burudani kwa Watanzania, kuwakumbusha Watanzania utamaduni wao, kutangaza utamaduni wa Watanzania sambamba na kusaidia Serikali kupitia sekta ya utalii kuongeza mapato.
Faridi ametoa wito kwa wanahabari kulitangaza tamasha hilo ili wadau wajitokeza kwa kulidhamini, hivyo kwa pamoja watakuwa wamesaidia kudumisha utamaduni wetu na kuisaidia serikali yetu kutunza utalii.
Chanzo: Michuzi Blog

No comments:
Post a Comment