Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, October 20, 2026

MCHENGERWA: DAWA BANDIA NI UHALIFU DHIDI YA WANANCHI

 

Na Happyness Hans, WAF - Dodoma

Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa (Mb), ameitaka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kuimarisha udhibiti wa dawa bandia na bidhaa za afya zisizokidhi viwango, akisema bidhaa hizo zinahatarisha maisha ya wananchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA, uliofanyika jijini Dodoma Oktoba 19, 2026, Mhe. Mchengerwa amesema udhibiti madhubuti unahitaji ujasiri, weledi na uadilifu, huku usalama wa wagonjwa ukipewa kipaumbele katika kila uamuzi. Amesisitiza kuwa TMDA inapaswa kukataa bidhaa au maombi ya usajili yasiyothibitisha usalama na ubora kwa mujibu wa ushahidi wa kisayansi, bila kujali ushawishi wa wawekezaji.

“Mdhibiti anayeogopa si mdhibiti; ni mhuri,” amesisitiza, akieleza umuhimu wa mamlaka hiyo kufanya maamuzi huru yanayolinda maslahi ya umma.

Ili kukabiliana na changamoto hiyo, ameitaka Bodi kusimamia uimarishaji wa ukaguzi wa bidhaa za afya sokoni na matumizi ya teknolojia.

No comments:

Post a Comment