DULLY SYKES AWAFUNGUKIA WAKONGWE WENZAKE
Inawezekana ukawa umesikia sikia stori za baadhi ya wasanii wakubwa wa
Tanzania kutopenda maendeleo au mafaniko ya wasanii wapya wanaofanya
vizuri this time.
Dully Sykes amekua msanii wa kwanza kujitokeza wakati huu na kukemea
wasanii wakubwa wenye tabia hizo.
Amesema “Hilo lipo wazi, msanii kama mimi nasikia raha sana vijana
kama Diamond, Tunda Man, Mr Blue, Ally Kiba na wengine wakifanya
vizuri, kwa hiyo msanii mkubwa kama utakua umeshindwa kufanikisha kile
ulichotakiwa kukifanya alafu kijana mdogo akafanya basi mpigie makofi,
kama unaona huwezi kufika pale unapotaka basi waachie vijana wafike,
tusiwaingilie”
Kuhusu uwepo wa wasanii wakubwa wenye wivu kwa wadogo wenye mafanikio,
Dully kasema “Wivu utakuepo unajua huwezi kuona kijana kaanza juzi tu
alafu leo anafanya kitu kizuri ukafurahia lakini sijui mimi nina moyo
gani tofauti na wenzangu, nafurahia sana vijana wakifanya vizuri kama
Diamond, Linah, Amini, Barnaba na wengine wanaofanya vizuri”
Kwenye line nyingine Dully amesisitiza kwa kusema “sioni sababu ya
mimi kumchukia mtu, sisi wasanii wakongwe wazee ambao tupo kwenye game
siku nyingi, tufurahie kazi ya vijana wanayoifanya tumfurahie Diamond,
Barnaba, Amini, Mr Blue na wengine wote, tuwafurahie wale…….. na sio
kwamba nimemsema mtu wala kumlenga mtu”
No comments:
Post a Comment