Mwenge wa Olimpiki Ukiwa Umefika Mbele ya Lango la Uwanja Wa
Olimpiki Tayari kwa kufunguliwa Masihindano hayo Baada ya Mwenge wa huo Kuzunguka
kwa Siku 68 Kuzunguka Uingereza
Macho yote leo ni
huko London Uingereza kwenye sherehe za ufunguzi wa Mashindano ya Olimpic 2012
Ufunguzi huo wa saa Tatu ulioandaliwa na mshindi wa Tuzo za
Oscar Muongozaji wa Filamu ya Slumdog
Millionaire, Danny Boyle, Utaangaliwa na
Watu 60,000 kwenye uwanja Maalum wa mashindano hayo uliojengwa huko East End,
London na kuangaliwa kwenye Luninga na watazamaji zaidi ya Bilioni Moja Duniani
Kote.
Sherehe hizo zitarushwa kuanzia saa 3 usiku kwa saa za huko
ambapo ni saa sita usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Watazamaji watatakiwwa kuimba pamoja na watumbuizaji na kutengeneza picha ya aina yake kwenye tukio hilo kubwa litakalokaribisha wanamichezo 16000 kutoka
nchi 204 duniani.
Kutakua na ulinzi mkali kwenye mashimndano hayo unaotolewa
na kampuni ya ulinzi ya G4S
Mamlaka zinazohusika na kukabiliana na ugaidi zimesema
hakuna wasiwasi na matukio hayo huku waziri mkuu wa uingereza David Cameroon
akisema Olimpiki yenye kilikua kipaumbele chake
No comments:
Post a Comment