Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, August 1, 2012

AFARIKI KWA KUGONGWA NA GARI MBAGALA WILAYANI TEMEKE...!

 MTU mmoja amefariki baada ya kugongwa na gari wakati akitembea kwa miguu eneo la Mbagala rangi tatu wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Kimkoa wa Kipolisi Temeke, David Misime alisema ajali hiyo ilitokea juzi majira ya saa 8:00 mchana wakati akitembea kwa miguu barabarani katika eneo hilo.
Alisema gari namba T643AJT likiwa na tela lenye namba za usajili T173BMA, likiendeshwa na dereva, Petro Lupenza (28) mgonga mtu na kufariki papo hapo  wakati likitokea Mbagala langi tatu kuelekea Kibulugwa.
Misiime alisema marehemu huyo alitambulika kwa jina moja la Asha anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka (20-25) ambapo mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya Temeke.
Alibainisha kuwa chanzo cha ajali hiyo hakikufahamika mara moja hata hiyo, dereva wa gari hilo anashikiliwa na polisi  kwa upelelezi zaidi.

No comments:

Post a Comment